ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 24, 2017

BREAKING NEWS:- JPM AIVUNJA BODI YA UKAGUZI WA MADINI (TMAA), WAZIRI MUHONGO HAKUNA JINSI TENA.

Rais Magufuli aivunja Bodi ya Ukaguzi wa Madini (TMAA)
Rais John Magufuli aivunja bodi ya Ukaguzi wa Madini Tanzania kutokana na mapendekezo ya kamati ya Uchunguzi wa Makontena ya Mchanga wa Dhahabu.

"Nimeivunja bodi ya TMAA, na ninaagiza vyombo vya dola na Takukuru muwafuatilie muwafikishe kwenye mkono wa sheria"


Pia Mhe. Rais ameeleza sababu kwa nini alimfukuza kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa.

Amesema kuwa alichukua uamuzi huo kutokana na Profesa huyo kueleza Kamati ya Bunge kiasi ambacho kilikuwa kipo kwenye makontena ya dhahabu ambacho hakikuwa sawa.

Profesa Ntalikwa alifutwa kazi na Rais Magufuli siku chache baada ya kufanya ziara ya kushtukiza bandarini lakini hakubainsha iwapo kuna uhusiano kati ya ziara hiyo na kufutwa kwake Ntalikwa.
JPM Amtaka Waziri Muhongo Ajiuzuru

Rais wa John Magufuli amtaka Waziri wa Nishati na Madini, Professa Sospiter Muhongo achie nafasi yake.

"Ninampenda sana Professa Muhongo, lakini pia ni rafiki yangu, lakini kwenye hili naomba kajifikirie na haraka sana uachie ngazi"

Rais Magufuli amesema haya leo wakati akipokea taarifa ya kamati ya Uchunguzi wa Kontena wa Mchanga wa Dhahabu.





"Walifikiri ni wasomi sana, Sasa wasomi wenzao wame Wa-Proove Wrong" JPM                    "Walifanya hivyo, Kwa makusudi, Au kwa kutokujua ama hawajui Professional yao"- JPM

"Nilipoomba Dakika 5, Mimi niliondoka na wenzangu kuteta kidogo, kwamba ripoti hii haiwezi kupita hivi hivi, lazima tufanye kitu wakati tukisubiri ripoti nyingine"- JPM

 "Nimeivunja bodi ya TMAA, na ninaagiza vyombo vya dola na Takukuru muwafuatilie muwafikishe kwenye mkono wa sheria"- JPM

"Ninampenda sana Profesa Muhongo, lakini pia ni rafiki yangu, lakini kwenye hili naomba kajifikirie na haraka sana uachie ngazi"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.