ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 11, 2017

BENKI YA KILIMO YAOMBWA KUTOA MIKOPO ARUSHA



Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega akihimiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (hayupo pichani) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha.
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kulia) akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki wakati akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga.
Meneja wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (kulia) akitoa takwimu za mahitaji ya mikopo ya mkoa wa Arusha. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji wa Biashara wa TADB, Bw. George Nyamrunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkabidhi muhtasari wa maeneo ya uwekezaji Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia).
Na Mwandishi wetu,           
Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuchangamkia fursa za uwekezaji katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo wakulima wanaojishughulisha katika sekta hizo mkoani Arusha ili kuchagiza sekta ya kilimo mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na ufugaji.
Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.
Bw. Assenga mkoa wa Arusha utaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.