ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 31, 2017

BADO HAIJAJULIKANA NINI KILICHOMUUA NDESAMBURO.

Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Bazil Lema amesema mwili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi mjini Phillemon Ndesamburo unafanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake cha ghafla.
Akizungumza leo, Lema amesema Ndesamburo alifika ofisini kwake asubuhi  kama ilivyo kawaida yake  lakini aliugua ghafla mnamo saa nne asubuhi.

Bazil alisema baada ya Ndesamburo kujisikia vibaya, alichukuliwa na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC na wakati madaktari wanakifanya jitahada za kumpa matibabu alifariki dunia.

“Baada ya mwili kufanyiwa uchunguzi taarifa rasmi kuhusu kifo chake zitatolewa na uongozi wa chama pamoja na familia,” amesema

Wakati huo huo wanachama wa Chadema wamekusanyika kwa makundi katika eneo la hospitali wakionekana kuwa sura za huzuni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.