ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 10, 2017

ASKARI 4 WA KULINDA AMANI WA UN WAUAWA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI.


Askari 12 wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa MINUSCA wameuawa na kujeruhiwa baada ya msafara wa magari yao kutekwa nyara na kushambuliwa na genge la waasi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Stephane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema wanajeshi wanne wa UN wameuawa huku wanane wakiachwa na majeraha mabaya, baada ya kuzuka makabiliano kati yao na kundi la waasi wa Kikristo la Anti-Balaka, karibu na eneo la Bangassou, yapata kilomita 474 mashariki mwa mji mkuu, Bangui Jumatatu usiku.

Amesema mbali na mauaji na majeraha hayo, askari mmoja wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoweka na hatima yake haijulikani hadi sasa.

Wapiganaji wa Kikristo wa Anti-Balaka huko CAR
Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres ametoa taarifa ya kulaani mashambulizi hayo dhidi ya maafisa wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, akisisitiza kuwa kuhujumiwa askari wa umoja huo ni sawa na jinai za kivita.
 Mapigano ya hivi karibuni katika miji ya Bambari, Ouaka, Mkoa wa Kati na Makoum, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mbali na kuua makumi ya raia, yamesasabisha maelfu ya raia wa nchi hiyo kukimbilia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya Rais François Bozizé.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.