ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 11, 2017

ZUMA AYATAJA MAANDAMANO YA AFRIKA KUSINI DHIDI YAKE KUWA NI YA KIBAGUZI.


RAIS Jacob Zuma wa Afrika Kusini leo ameyataja maandamano ya wiki iliyopita nchini humo ya kumshinikiza ajiuzulu kuwa ni ya kibaguzi. 
Makumi ya maelfu ya wananchi Ijumaa iliyopita waliandamana katika miji mbalimbali ya Afrika Kusini kudhihirisha hasira zao kutokana na kashfa mbalimbali za ubadhirifu, ukosefu wa ajira na kuzorota uchumi chini ya utawala wa Rais Zuma. Hatua ya Zuma ya kumfuta kazi Pravin Gordhan Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini aliyekuwa akiheshimika nchini humo imeibua upinzani na malalamiko mapya ya wananchi na kutoka kwa shakhsia wa ngazi ya juu wa chama tawala ANC, akiwemo Makamu wa Rais.
Maandamano dhidi ya Rais Zuma  
Rais Jacob Zuma amesema kuwa maandamano ya wiki iliyopita yamedhihirisha kuwa ubaguzi upo huko Afrika Kusini. 
 
Amesema mabango na maberamu yaliyobebwa na waandamanaji yalidhihirisha imani ambazo amesema walidhani zilishatokomezwa, huku mabango mengine yakiwa yamechorwa raia weusi na kuwaonyesha kuwa ni nyani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.