ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 19, 2017

WAVUVI WA LIBYA WAWAKUTA PWANI WAHAJIRI 28 WAKIWA WAMEKUFA


Wavuvi wa Libya wamepata miili ya wahajiri 28 katika pwani ya nchi hiyo ambao wanasadikiwa kuwa waliaga dunia kutokana na kiu na njaa, baada ya boti yao kupasuka katika pwani ya mji wa Sabratha. Hayo yameelezwa na afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya. 
Tangu Libya itumbukie machafukoni baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi apinduliwe mwaka 2011, nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika imekuwa kituo kikuu zinapoanzia safari za wahajiri wanaoelekea Ulaya kwa njia ya bahari. 

Wahajiri zaidi ya 150,000 wamefanikiwa kutumia njia hiyo ya bahari na kuingia Italia katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Eneo la pwani ya Sabratha ambako miili ya wahajiri hao imepatikana  
Ahmaida Khalifa Amsalam Kamanda wa Kitengo cha Usalama katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa baada ya kuzama jua wavuvi waliwakuta wahajiri hao 28 wakiwemo wanawake wanne wakiwa wameaga dunia katika pwani ya mji wa Sabratha. Ameongeza kuwa wahanga hao wamezikwa pamoja katika kaburi mahsusi la wahamiaji haramu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.