ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 3, 2017

WATOTO 43 NI MIONGONI MWA WALIOFARIKI KWENYE MAPOROMOKO YA UDONGO COLOMBIA.


RAIS Juan Manuel Santos wa Colombia ametangaza kuwa watoto 43 ni miongoni mwa watu 254 waliofariki katika mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyotokea nchini humo.
Rais Santos ameyasema hayo wakati alipotembelea mji wa Mocoa kusini mwa nchi hiyo ambapo mbali na kuthibistiha takwimu zilizotolewa kuhusu idadi ya waliofariki amesema kuna uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka.

Rais wa Colombia aidha amehimiza kuongezwa kasi ya operesheni ya uokozi na utoaji misaada na pia ametoa mkono wa pole kwa familia zilizopoteza watu wao katika janga hilo.


Rais Juan Manuel Santos alipotembelea eneo la maafa
Mbali na watu 254 walioripotiwa hadi sasa kufariki dunia, wengine wasiopungua 400 wamejeruhiwa na maelfu wamelazimika kuyahama makaazi yao.

Maafisa wa sekta ya afya ya Colombia wamesema jitihada zinafanyika ili kuepusha kutokea magonjwa ya kuambukiza kufuatia tukio hilo la mafuriko na maporomoko ya udongo. Wakati huohuo kundi la zamani la waasi la FARC limetangaza kuwa wanamgambo wake wako tayari kusaidia kujenga upya mji wa Mocoa.

Maeneo mengi ya mji huo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko na maporomoko hayo ya udongo ni ya watu masikini ambayo wakaazi wake walipoteza makazi yao na kulazimika kuwa wakimbizi wakati wa miongo mitano ya vita vya ndani nchini humo.Juhudi wa uokozi zikiendelea
Maporomoko ya udongo yaliyotokana na mvua kali zilizonyesha kwa muda wa siku kadhaa nchini Colombia na kusababisha kufurika kingo za mito mitatu ya nchi hiyo, mbali na maafa ya roho za watu yamesababisha pia hasara kubwa kwa nyumba, magari, madaraja na miti.
 
Itakumbukwa kuwa, watu zaidi ya 20 elfu walipoteza maisha katika maporomoko mengine ya ardhi yaliyotokea nchini Colombia mwaka 1985 katika eneo la Armero

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.