ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 20, 2017

VIONGOZI WA UPINZANI ZIMBABWE KUUNGANA ILI KUPAMBANA NA RAIS MUGABE KATIKA UCHAGUZI 2018


Wapinzani wawili wakuu wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wamesema wameamua kuungana ili kuhakikisha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 haendelei kubaki tena madarakani kwa muhula mwengine wa miaka mitano.
Morgan Tsvangirai, kiongozi wa chama cha MDC-T ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa serikali tete ya mseto iliyoongozwa na Rais Mugabe kuanzia mwaka 2009 hadi 2013 amesema yeye na Bi Joice Mujuru, ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Mugabe hadi alipotimuliwa mwaka 2014, watapigania kuunda serikali ya mseto ili kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo.
"Huu ni mwanzo tu wa kuweka msingi kuelekea uundaji wa muungano mpana zaidi wa kupambana na ZANU PF kuanzia sasa hadi uchaguzi ujao mwaka 2018", ameeleza Tsvangirai akikusudia chama tawala kinachoongozwa na kiongozi huyo mzee zaidi kiumri barani Afrika.
Rais Robert Mugabe
Chama hicho tawala nchini Zimbabwe ambacho kinaiongoza nchi hiyo tangu ipate uhuru wake mwaka 1980, mwezi Desemba mwaka jana kilimpitisha rasmi Mugabe kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi unaotazamiwa kufanyika katikakati ya mwaka ujao ambapo kiongozi huyo atakuwa ametimiza umri wa miaka 94.
 
Bi Majuru ambaye mwaka jana aliunda chama kipya cha Taifa cha Wananchi amesema vyama vyao viwili vya upinzani vimekuwa vikijadiliana kwa muda wa miezi sita ili kufikia makubaliano na kwamba sasa wanatarajia kuanza mazungumzo ya kina juu ya masuala maalumu ili kuimarisha muungano wao.
Wapinzani wanamlaumu Rais Mugabe kwa kuua uchumi wa Zimbabwe ambayo ni moja ya nchi za Kiafrika iliyokuwa na ustawi mkubwa; hata hivyo chama chake kinasema uchumi wa nchi hiyo umedhoofishwa na madola ya Magharibi

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.