ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 19, 2017

TRUMP AAMURU KUANGALIWA UPYA MAKUBALIANO YA JCPOA

Rais Donald Trump wa Marekani ameiagiza kamisheni ya usalama wa taifa ya nchi hiyo kuangalia upya makubaliano kwa jina la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Rex Tillerson Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amesema kuwa Trump ameitaka kamisheni ya usalama wa taifa ya nchi hiyo ichunguze iwapo hatua ya Rais msaafu wa nchi hiyo Barack Obama ya kuifutia vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa kwa maslahi ya Washington au la. Itakumbukwa kuwa akiwa katika kampeni za uchaguzi wa rais mwaka jana, Trump aliyataja makubaliano ya JCPOA kuwa ni maafa na makubaliano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa duniani na kuahidi kuwa, angeyachana katika siku yake ya kwanza ya kuanza kazi huko White House.  

Jamii ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Ulaya zimekiri kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza ahadi zake zote katika fremu ya makubaliano hayo, hata hivyo Marekani imekuwa ikifanya kila linalowezekana kukwamisha makubaliano hayo ya kimataifa. Federica Mogherini Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya hivi karibuni naye alisisitiza kuwa makubaliano ya  JCPOA ni milki ya jumuiya za kimataifa na kwamba si makubaliano ambayo yanaweza kuratibiwa na pande mbili tu na kufanyiwa mabadliko na pande hizo.

Federica Mogherini, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.