ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 23, 2017

NANI KUIBUKA KIDEDEA KITI CHA URAIS UFARANSA.

Wagombea maarufu (Kushoto kuenda kulia): François Fillon, Benoît Hamon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron na Jean-Luc Mélenchon

Raia wa Ufaransa wanapiga kura ya urais hivi leo.
Kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa , huu umekuwa uchaguzi usiotabirika.
Takriban asilimia 30 ya wapiga kura wanaaminika kwamba hawajatangaza msimamo wao.

Wawaniaji watatu wakuu hawana historia yoyote ya kisiasa akiwemo Emmanuel Macron, Marine le Pen na Jean-Luc Melenchon
Mpinzani wao mhafidhina Francois Fillon, amehudumia serikali katika nyadhfa kadhaa za uwaziri katika kipindi cha miongo miwili.
Hali ya usalama imeimarishwa mara dufu, karibu polisi 50,000 na wanajeshi 7,000 wametumwa kote nchini.

Hakuna yeyote anayetarajiwa kuibuka na ushindi katika duru ya kwanza, na wawili watakaoongoza uchaguzi huo watamenyana na katika duru ya pili mwezi ujao.
Usalama umeimarishwa kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea katikati mwa mji mkuu Paris alhamis, ambapo afisa mmoja wa polisi aliuwawa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.