ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 11, 2017

MWAUWASA YAJA NA MFUMO WA KUWABANA WALIPAJI WA ANKARA ZA MAJI

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

KUFUATIA kuwepo kwa madeni ya ankra ya maji kwa taasisi za umma Mamlaka ya  Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa) imesema inajipanga kununua  mashine maalumu za luku ambazo zitafungwa kwenye taasisi za umma zilizounganishiwa huduma ya maji ili kuepuka madeni.

Mamlaka hiyo imesema   lengo la mashine hizo ni kudhibiti na kuepuka madeni ya taasisi za umma ambazo zimekuwa zikitumia maji mengi huku zikishindwa kulipa ankara jambo ambalo linasababisha Mwauwasa kushindwa kujiendesha na kufikia malengo ya kila mwaka.

Akizungumza na G sengo blog  Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano wa Mwauwasa,  Oscar Twakazi kwa niaba ya  Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Antony Sanga, ambapo ameeleza kuwa licha ya mpango huo kuanza na wateja wakubwa ambao wamekuwa wasumbufu katika ulipaji wa ada za maji lakini pia utawahusisha wananchi.

Amesema mpango huo unatarajia kuanza mwaka wa fedha ujao 2017/2018 ili kuweka mfumo unaojulikana kwa jina la “malipo kabla ya matumizi”,utakao saidia kumbana mtumiaji wa maji kwa kununua kila anapohitaji.

Twakazi amesema mfumo huo utakawa suluhisho kwa taasisi za umma ambazo zimezoea kutumia maji mengi ya mamlaka  bila kulipa ankara na hata wanapotengewa fedha kutoka hazina, huzitumia kwa mambo mengine.

“Hizi taasisi za umma tunazidai Sh bilioni mbili ikilinganishwa na Sh milioni 300 za wateja wa kawaida, tumekaa na kuona tukija na mfumo wa malipo kabla ya matumizi tutakuwa tumekomesha suala la taasisi hizi kutolipa ankara za maji.

“Ingawa mashine hizi ni gharama kubwa kwani moja inagharimu Sh milioni 50 lakini tutazinunua chache na kuzifunga kwenye taasisi zile zinazotumia maji mengi na kushindwa kulipa, kwa kufanya hivyo tutaepusha mvutano maana zipo taasisi zingine ukitaka kwenda  eneo lao ni shida,”amesema Twakazi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.