ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 11, 2017

MWAUWASA WANADAI BIL 2 TAASISI ZA UMMA.

Jiji la Mwanza.
NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mwanza imesema inazidai taasisi za umma Sh bilioni mbili huku wateja wa kawaida wakidaiwa Sh million 300

Akizungumza na G sengo Blog Kaimu Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Oscar Twakazi kwa niaba ya Mkurugenzi Mhandisi Antony Sanga amesema wanatekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kusitisha utoaji wa huduma kwa wadaiwa  sugu wa ankara za maji zikiwamo taasisi za umma na binafsi.

Twakazi amesema  kuhusu wateja ambao wapo katika daraja la kawaida, tayari wameikabidhi kampuni ya Sai Soliciators & Avocates majina ya waidaiwa wote ili kukuksanya fedha hizo  kabla ya kufikia uamuzi wa kusitisha huduma kwao.

“Hapa kuna wateja wetu aina tatu, wateja wa kaiwada, kampuni na viwanda sambamba na taasisi za umma, sasa kwa upande wa wateja wa kawaida tunawadai Sh milioni 300 ambazo zitakusanywa na Sai Soliciators & Avocates.

“Kwa upande wa kampuni na viwanda hatuna shida nao maana ni walipaji wazuri, tatizo lipo kwenye taasisi za umma Mpaka sasa Mwauwasa inawadai Sh bilioni 2, tunatarajia kuwapo kwa ‘notes’ ya kulipa madeni yao, lakini tumewasiliana na hazina makao makuu juu ya madeni yao na wametuelekeza kwamba tuhakikishe madeni hayo upya na kuwapelekea wao ili waweze kuingiza fedha hizo moja kwa moja kwetu,”amesema.

Twakazi amesema kwamba  baada ya kufanya mawasiliano na hazina, wamebaini kuwa taasisi za umma ambazo zinadaiwa na Mwauwasa zilikuwa zikipewa fedha lakini hazikuona umumhimu  wakulipa badala yake walizitumia kwa mambo mengine ambayo waliyaona ni kipaumbele kwao.

Akizungumzia tatizo lilitokeza takribani wiki mfululizo la kutokuwapo kwa uhakika wa maji jijini Mwanza, amesema lilitokana na hitilifafu ya umeme  iliyojitokeza kwenye kituo kikuu cha kuzalishaji maji eneo la Kapri point.

“Kulijitokeza hitilafu ya umeme katika chanzo chetu cha maji jambo lililosababisha  mitambo kuzima mara kwa mara, fundi wetu wamepiga kambi huko na tayari wamefanikisha kurejesha hali vizuri na kazi inayoendelea sasa ni kusukuma maji kwenye  matenki yetu, tunaomba wananchi wawe watulivu huduma itarejea kama kawaida,”alisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.