ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 24, 2017

MMOJA AJINYONGA HADI KUFA KWA KUTUMIA KAMBA YA KATANI WILAYANI NYAMAGANA CHANZO BADO UTATA.


Mtu mmoja mwanaume aliyefahamika kwa jina la Faraja Anselem (31), mkazi wa mtaa wa Mkuyuni Sokoni, amekutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani aliyokuwa ameifunga kwenye paa la chumba chake.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea jana jioni majira ya saa 18:45

Inasemekana kuwa marehemu siku ya tukio alibaki mwenyewe nyumbani, aidha inadaiwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo marehemu alionekana kuingia chumbani kwake kisha akafunga mlago ndipo baada ya muda kupita watoto waliokuwa wakicheza jirani na maeneo hayo, kupitia dirisha la chumba hicho waliona miguu ikining'inia ndipo walipotoa taarifa kwa wazazi wao.

Majirani baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu ukining'inia mahali hapo.
Kamanda Msangi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi pindi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi. Aidha uchunguzi kuhusiana na kifo hicho bado unaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kusaidiana kwa ukaribu pale watakapoona mtu anaonekana kuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi kupelekea kutaka kujidhuru yeye mwenyewe au watu wengine, wamfikishe kwa wataalamu wa ushauri nasaha ili aweze kupata msaada na kuondokana nahali hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.