ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 2, 2017

MLIPUKO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU WAIACHA PABAYA SOALIA.

KWA mujibu wa mkuu wa Idara ya Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Ulaya, Johan Heffinck, mwaka huu pekee kumeripotiwa kesi 18,000 za kipindupindu kote Somalia ambapo kwa kawaida kiwango hicho kuwa ni 5,000. Amesema kati ya wagonjwa 45 mgonjwa moja hupoteza maisha kutokana na kipindupindu nchini Somalia.

Aidha amesema ukame umepelekea Somalia kukumbwa na baa la njaa ambapo raia milioni 12 wa nchi hiyo watahitajia misaada kuanzia mwezi Julai. Anasema familia nyingi zinalizimika kutumia maji machafu kufuatia uhaba wa mvua uliossababisha mito na visima kukauka. 

Taarifa zinasema eneo lililojitenga la Somaliland lina hali mbaya zaidi kwani hakujashuhudiwa mvua eneo hilo tokea mwaka 2015. Hivi sasa mifugo mingi imefariki katika eneo ambalo utajiri wa watu ni mifugo.
Ukame Somalia

Mwezi Februari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema baa la njaa limeenea katika nchi kadhaa za Afrika na Yemen huku akisema hali ya Sudan Kusini ni mbaya sana.

Alibainisha kuwa watu zaidi ya milioni 20 Sudan Kusini , Somalia, Yemen , na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanakabiliwa na njaa na hawana uhakika wa kupata chakula. Alisema mashirika ya kutoa misaada yanahitaji angalau dola bilioni 4.4 ifikapo mwisho wa mwezi ulopita Machi ili kuepuka maafa.
Aidha Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, watoto takriban milioni 1.4 nchini Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa.

Katika taarifa, UNICEF imetoa wito kwa jamii ya kimataifa ichangie dola za kimarekani milioni 255 ili kukabiliana na hali hiyo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.