ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 1, 2017

MKUU WA WILAYA YA GEITA.,MWAL HERMAN KAPUFI AMEONGOZA MAMIA KUUHAGA MWILI WA ALIYEUWA MWAKILISHI WA CHANNEL TEN MKOA WA GEITA

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Valence Robart Mulamula ukiwa nje ya nyumba yao kwaajili ya heshima ya mwisho kabla ya kwenda kuzikwa kwenye makazi yake ya milele.
Baba wa Marehemu wa katika kati akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alifika kutoa pole na kushiriki mazishi.
Mkuu wa wilaya ya Geita akitoa pole kwa mama wa Marehemu Valence Robart.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi (katikati)akibadirishana mawazo na Mwenyekiti wa halmashauri ua mji wa Geita pamoja na mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita.
Mwili wa Marehemu Valence Robart ukitolewa Nje.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ,akitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Valence Robart.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji  Lernad Kiganga Bugomola akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa mwanahabari Valence Robart.
Mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita,Saimon akiaga mwili.
Mwandishi wa ITV Mkoani Geita,Rose Mweko akitoaga mwili wa marehemu Valence Robart.



Marehemu Valence Robert alianza kusumbuliwa na maradhi mwaka jana mwishoni na katika juhudi za kutafuta matibabu alipelekwa jijini mwanza ambapo  alipatiwa matibabu na kurudia hali yake ya awali na kuendelea na Majukumu yake ya kazi lakini Mwanzoni mwa mwaka huu mwezi wa pili hali yake ya afya ilibadirika na kupelekea kuzidiwa mwezi wa tatu hali ambayo ilimrazimu kurudi Nyumbani kwaajili ya matibabu.

Kwa Mujibu wa Mzazi wake wa Kiume ,Mzee Robert Mulamula alisema kuwa hali yake ilibadirika ghafra siku ya juma nne ya tarehe 28 na walipo kuwa katika jitihada za kutaka kumkimbiza hospitali hali ilibadirika na kupelekea kukata kauli .

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwilimu Herman Kapufi amewataka wazazi kuwa na Moyo wa subira na kuachana na dhana ambazo zimekuwa zikiibuka pindi mtu anapofariki kuwa amelogwa na kwamba jambo hilo sio la kweli kwani marehemu alikuwa ni mgonjwa kama ambavyo wengine wamekuwa wakiugua.

Akimwakilisha Mbunge wa viti maalum kwa Tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Mkoani Geita Upendo Peneza  katibu wake Shida Mpondi alisema kuwa mbunge huyo ameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani marehemu Valence Robart alikuwa ni mtu wa karibu ambaye walikuwa wakishirikiana katika kazi za ujenzi wa Taifa.

Hata Hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola ,aliwaasa wanajamii ,ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu kuendelea kujikabidhi mikononi mwa Mungu kwani hayupo hajuae siku wala saa ya kuondoka Duniani.

Marehemu  Valence Robart wakati wa uhai wake ameshawai kuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten na gazeti la Tanzania daima Mkoani Geita.

Na alizaliwa Tarehe 9mwezi wa 11 mwaka 1986 katika kijiji cha Mugana Wilayani Misenyi Mkoani Kagera akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya mzee Robart Mulamula na alifariki tarehe 28 mwezi wa 3 mwaka 2017.

Siku ya jana ya tarehe 30 mwezi wa March mwaka huu  amezikwa katika kijiji ambacho amezaliwa.

Kwa niaba ya wasomaji wa Mtandao wa Maduka Online inatoa pole kwa familia kwa kuondokewa na kijana wao Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake ribarikiwe.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.