ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 11, 2017

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKAJI KUZINDUA KLABU ZA ELIMU YA UZIMAJI MOTO SHULE ZA SEKONDARI NCHINI



Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kueleza mipango mbalimbali ya jeshi hilo ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi, Casmir Ndambalilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa kuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, akiuliza swali kwa Kamishna Jenerali wa jeshi hilo,Thobias Andengenye (hayupo pichani), wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa kuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye  wakati wa mkutano huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.