ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 30, 2017

MAN U YALAZIMISHWA SARE NA SWANSEA CITY, ARSENAL YAGAGADULIWA NA TOTENHAM, CHELSEA WALEEEE KILELENI.


Viongozi wa wa Ligi ya Premier Chelsea walipiga hatua kubwa kuelekea kushinda ligi baada ya kuwanyuka Everton mabao matatu kwa nunge.
Mabao yote ya Chelsea yalifungwa katika kipindi cha pili.

Ina maana kuwa hata kama Chelsea itashuka kwa pointi tatu kwenye mechi nne zilozosalia bado itachukua nafasi ya pili kwa miaka mitatu mfululizia hata kama Tottenham watashinda mechi zote zilizosalia.

Iliwalazimu Chelsea kusubiri kabla ya kombora ya Petro lililotumbukia wavuni mnamo dakika ya 66.

Everton walikuwa wameanza kwa kasi kwa mwendo wa kazi ambapo Dominic Lewin nusura afunge.

Sare ya Manchester City na Middlesbrough ina maana kuwaa klabu yake Ronald Koeman iko nyuma kwa pointi nane kutoka kwa klabu nne za kwanza huku ikibaki na mechi tatu tu.

 Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford akienda chini baada ya kuangushwa na kipa wa Swansea City, Lukasz Fabianski na refa Neil Swarbrick kuamuru penalti ambayo ilifungwa na Wayne Rooney kuipatia timu yake bao la kuongoza dakika ya 45 na ushei katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford, kabla ya wageni kusawazisha kupitia kwa Gylfi Sigurdsson dakika ya 79.

VIDEO 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.