ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 6, 2017

A-Z KUKAMATWA KWA ROMA.

Msanii Roma Mkatoliki

CHANZO: MUUNGWANA BLOG
Baada ya kuzagaa kwa taarifa kuhusu kukamatwa kwa Msanii Roma Mkatoliki akiwa studio na kupelekwa kusiko julikana, Muungwana Blog imefika katika studio za Tongwe Records jijini Dar es salaam ambapo mkasa mzima ulikuwa hivi...

Kwa mujibu wa Mashuhuda (Majina yanahifadhiwa) walio ambao pia wanaishi katika nyumba ambayo inapatikana studio ya Tongwe, wameijuza Muungwana kuwa April 5, 2017 ambayo ilikuwa ni jana, katika majira ya Saa moja jioni ilionekana gari aina ya Noah nyeusi nje ya studio hizo, ambapo walishuka watu zaidi ya Watano na kuingia ndani ya  studio hizo.

Watu hao bila ya kujitambulisha walitamka kuwa wanamuhitaji Roma na mwenzake ambapo walimchukua na kutoka nae nje, na baada ya muda kidogo walirejea ndani na kuwachukua wengine watano akiwemo na Prodyuza wa studio hiyo Anayeitwa Moni.

Mbali na kuwachukua watu hao pia mashuhuda hao wemeeleza baadhi ya vifaa vya studio hiyo pia vimebebwa ikiwemo TV, na Computer.

Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Studio hiyo  aliyejitambulisha kwa jina moja la Edin ameiambia Muungwana Blog kuwa nikweli tukio hilo limetokea na mpaka sasa hawajui Roma na wenzake wamepelekwa wapi na hivyo hawezi kuelezea zaidi mpaka atakapojua walipo wakina Roma, ambapo aliongeza kuwa anakwenda kuripoti katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini humo.

Hata hivyo saa chache baada ya tukio hilo kumekuwa na tetesi kuwa huenda kuvamiwa kwa studio hizo kumesababishwa na nyimbo  ya Tanzagiza ambayo imeachiwa hivi karibuni na Msanii Sifa Digital ambapo mwanzoni tu wa nyimbo hiyo linasikika jina la studio ya Tongwe Records huku maudhui ya nyimbo hiyo yaneikashifu serikali.

Hata hivyo uongozi wa Tongwe Records umekana kuwa kuhusika na utengezwaji wa nyimbo hiyo na kwamba msanii huyo ametumia "beat" ya Studio hizo bila wao kujua.
 Mkurugenzi wa Tongwe Records Junior Makame 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tongwe Records Junior Makame mnamo march 27, 2017 aliandika hivi kupitia ukurasa wake wa Instagram

"Sisi kama wanafamilia  na uongozi mzima wa TONGWE RECORDS tunasikitishwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kutumia midundo/ beats / instrumentals zetu za nyimbo zilizotoka kwa ajili ya kutengenezea nyimbo zao za kampeni wanazozijua wao wenyewe pasipo idhini yetu.. Tunaomba ambao washafanya hivyo wazuie kusambazwa kwa nyimbo zao hizo mara moja ili kutuepusha na lawama zitakazoletwa baada ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria kwa kukiuka haki zetu za kikatiba. 

Wenu ktk ujenzi wa taifa 
Junior ' J- Murder ' Makame. Oi"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.