ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 6, 2017

WATU TISA (09) WAMEJERUHIWA KATIKA VURUGU WAKATI WA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO SEHEMU ZISIZO RUHUSIWA WILAYANI NYAMAGANA.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 06.03.2017


·         WATU TISA (09) WAMEJERUHIWA KATIKA VURUGU WAKATI WA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO SEHEMU ZISIZO RUHUSIWA WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 05.03.2017 MAJIRA YA SAA15:45HRS KATIKA MTAA WA BUHONGWA CENTER WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU TISA AMBAPO  ASKARI MGAMBO WA JIJI LA MWANZA SABA (07), AFISA MAZINGIRA MMOJA (01) NA DEREVA WA JIJI MMOJA (01) WALIJERUHIWA KWA KUPIGWA NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI MIILI YAO NA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO WALIOKUWA WAKIFANYA BIASHARA PEMBENI YA BARABARA WAKISHIRIKIANA NA WATU WENGINE WALIOKUA WAKISHABIKIA WAKATI WAKIENDELEA NA ZOEZI LA KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA WADOGOWADOGO KATIKA MAENEO YASIYO RUHUSIWA HASWA KWENYE HIFADHI YA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA.

MGAMBO WALIOJERUHIWA NI 1. NDAISABAS NICODEMU  MIAKA 25, MKAZI WA MKUYUNI, AMBAYE AMEJERUHIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA HALI YAKE BADO SIO NZURI, 2. ALEX JOSEPH MIAKA 25, MKAZI WA ISAMILO, AMBAYE AMEVUNJIKA MGUU WA KULIA KWENYE PAJA, 3.EMMANUEL BIGAMBO MIAKA 37, MKAZI WA PASIANSI, AMBAYE AMEUMIA KIUNO, 4.ASIFIWE ANDREA MIAKA 33, MKAZI WA IGOGO , AMBAYE AMEUMIA GOTI MGUU WA KULIA, 5. DAVID BAKARI MIAKA 32, MKAZI WA NYAMANORO, AMBAYE AMEUMIA MGUU WA KULIA KWENYE GOTI, 6.ZACHARIA ANDREA MAIAK 24, MKAZI WA MKOLANI, AMBAYE AMEUMIA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA NA KIDOLE GUMBA CHA MKONO WA KUSHOTO NA 7.SURUSI JOSEPH MIAKA 21, MKAZI WA KILOLELI AMBAYE AMEUMIA KIWIKO CHA MKONO WA KUSHOTO.

WENGINE NI 8.FANUEL KASENENE MIAKA 39, AFISA MAZINGIRA WA JIJI LA MWANZA NA MKAZI WA NYEGEZI, AMBAYE AMEJERUHIWA JUU YA JICHO LA KUSHOTO NA MDOMONI NA 9.GHARIBU AHAMADI MIAKA 32, DEREVA WA JIJI NA MKAZI WA NYAKATO, AIDHA KATIKA VURUGU HIZO KULIFANYIKA UHARIBIFU WA GARI LA HALMASHAURI LENYE NAMBA DFPA 2387 AINA YA SINO AMBALO LILIVUNJWA VIOO.

AIDHA WAKATI VURUGU HIZO ZINAENDELEA WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI AMBAPO ASKARI WALIFIKA KWA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUDHIBITI VURUGU HIZO. AIDHA KATIKA HARAKATI ZA KUDHIBITI VURUGU HIZO ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU TISA AMBAO INADAIWA KUWA WALIKUWA WAKIHUSIKA KATIKA VURUGU HIZO, JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE TISA NA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI WOTE WAPO HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO INAENDELEA VIZURI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO AKIWATAKA KUTII SHERIA BILA SHURUTI ILI KUEPUSHA MAJERAHA NA VURUGU ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANAWATAKA PIA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BALI PINDI WANAPOKUWA NA MALALAMIKO WATEUE VIONGOZI AMBAO  WATAPELEKA MALALAMIKO YAO KWA UONGOZI HUSIKA ILI YAWEZE KUTATULIWA KWA AMANI.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.