ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 27, 2017

WANAJESHI WA KENYA WAANGAMIZA WANAMGAMBO 31 WA AL SHABAB.


WANAJESHI wa Kenya nchini Somalia wamewauwa wanamgambo 31 wa kundi la kigaidi la al Shabab katika shambulio walilofanya katika kambi mbili za kundi hilo huko Jubbaland kusini mwa Somalia. Hayo yameelezwa leo Jumatatu na jeshi la Kenya. 
Nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika ina maelfu ya wanajeshi wake wanaohudumu katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika huko Somalia kwa kifupi (AMISOM). 

Wanajeshi hao wa Kenya walitumwa Somalia kusaidia kuwaangamiza wanamgambo wa al Shabab na kuboresha hali ya usalama kama sehemu ya kuijenga upya Somalia baada ya kuathiriwa na vita vya ndani vya miongo miwili vilivyoidhoofisha pakubwa nchi hiyo.
Jeshi la Ulinzi la Kenya limeeleza kuwa wanajeshi wao wa nchi kavu walisaidiwa na helikopta na mizinga kuwashambulia al Shabab. Jeshi la Kenya pia limefanikiwa kukamata silaha kadhaa, zana za mawasiliano na sare za jeshi katika shambulio hilo dhidi ya kundi la kigaidi la al Shabab huko Jubbaland.
Helikopta za Kenya katika oparesheni dhidi ya al Shabab

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.