ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 28, 2017

UN: WATOTO 1400 WAMEUAWA NCHINI YEMEN.


TAARIFA iliyotolewa na Stephen O'Brien imesema kuwa, maelfu ya raia wa Yemen wameuawa katika vita vya nchi hiyo na kwamba 1400 kati yao walikuwa watoto.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, thuluthi moja ya jamii ya watu wa Yemen inahitaji misaada ya kibinadamu.

Wakati huo huo Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umeashiria vita vinavyoendela kwa miaka miwili sasa nchini Yemen na kutangaza kuwa: Watoto laki tano nchini humo wanakabiliwa na hatari kubwa ikiwa ni pamoja na njaa na uhaba wa maji.
UNICEF imezitaka pande zote na jamii ya kimataifa kufanya jitihada za kuzuia maafa ya baa la njaa nchini Yemen na kukidhi mahitaji ya raia wanaoteseka wa nchi hiyo.

Mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia ikisaidiwa na Marekani na washirika wao dhidi ya watu wa Yemen yameua maelfu ya raia wasio na hatia na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.