ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 10, 2017

TAMASHA LA BATTLE ZONE LAJA MWANZA


Mkurugenzi wa Kampuni ya White Fish Entertainment (Katikati) Frank Mnubi akizungumza na wanahabari kuhusu Tamasha la Battle Zone katika Ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.Tamasha la Battle Zone lafanyika Pasaka Rock City Mall
Na James Timber, Mwanza
Tamasha la Battle Zone lapangwa kufanyika Aprili 16, mwaka huu katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Rock City Mall Mkurugenzi wa Tamasha hilo kupitia Kampuni ya White Fish Entertainment Frank Mnubi alisema kuwa ameandaa tamasha kwa lengo la kuinua na kukuza vipaji kwa mkoani hapa na mikoa jirani.

Mnubi alisema kwa wale wanaotaka kujiunga na shindano hilo wafike katika ofisi ya White Fish Entertainment kwa ajili ya kujaza fomu ya ushiriki.

“Naomba vijana wafike katika ofisi ya White Fish Entertainment kwa ajili ya kuchukua fomu ya usajili, bila kujari jinsia wala sehemu atokayo,” alisema Mnubi.
Alisema kuwa wasanii wanaotakiwa wamegawanyika makundi mawili kundi la awali ni wanaofanya muziki wa kufoka (Hip Hop) na lingine ni kwa wale wanaocheza (Dancers).

Hata hivyo, alishukuru  Kampuni ya Simu ya Itel na kinywaji cha Coca cola kwa kudhamini tamasha hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.