ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 8, 2017

SNOWDEN: iPhone na ANDROID ZINATUMIWA NA CIA KUNASA MAZUNGUMZO YA WATU.


AFISA wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) amesema mifumo ya simu za iPhone na Android inatumiwa na vyombo vya ujasusi vya Marekani kudukua na kunasa sauti na mazungumzo ya watu katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Edward Snowden amesema maelfu ya nyaraka za siri za shirika la ujasusi la Marekani CIA zilizofichuliwa na mtandao wa WikiLeaks zimethibitisha tena kwamba mashirika ya ujasusi ya Marekani yanadukua na kunasa mazungumzo ya simu za kiganjani hususan zile zinazotumia mfumo wa iOS wa simu za  iPhone na ule wa Android.

Jumanne ya jana mtandao wa WikiLeaks ulichapisha sehemu ya kwanza ya nyaraka na mafaili ya siri ya shirika la ujasusi la Marekani CIA katika majmui iliyopea jina la Year Zero. Nyaraka hizo za siri zinafichua kuwa, CIA imekuwa ikifanya ujasusi wa kunasa na kusikiliza mazungumzo ya watu wanaotumia simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple na zile zinazotumia mifumo wa Android  na Microsoft na vilevile televisheni za Samsung kwa ajili ya kufanya ujasusi na kudukua sauti na mazungumzo ya watu katika pembe mbalimbali duniani.

Afisa wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) Edward Snowden anasema kufichuliwa nyaraka hizo kunathibitisha tena kwamba, mashirika ya ujasusi ya nchi hiyo yanajasisi na kunasa sauti za watumiaji wa simu za kiganjani.

Afisa huyo wa zamani wa NSA alikimbia Marekani mwaka 2013 akiwa na rundo kubwa la nyaraka za siri za mashirika ya ujasisi ya nchi hiyo na kwa sasa amepewa hifadhi nchini Russia. 
Edward Snowden.
Marekani imeitaka Russia kumkabidhi afisa huyo wa zamani wa NSA. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.