ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 6, 2017

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MTENDAJI MKUU WA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA.

RAIS Dk. John  Magufuli ametengua  uteuzi wa   Mtendaji  Mkuu wa Shirika  Elimu Kibaha  Dkt. Crspin  Mpemba  ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema kufuatia tuhuma mbalimbali za uendeshaji, zinazolikabili Shirika hilo ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa.

Simbachawene amesema Mnamo Machi, 4 mwaka huu Rais Magufuli ametengua  rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

Amefafanua kuwa kumekuwepo  malalamiko dhidi ya Mtendaji  Mkuu wa  wa shirika la Elimu Kibaha ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI  iliunda kikosi kazi  ili kufanya uchunguzi dhidi ya malalamiko hayo na kugundua  kuwepo kwa changamoto katika uendeshaji wa Shirika hilo.

 “Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja  zinazohitaji uchunguzi zaidi,” ameeleza Waziri Simbachawene.

Ameongeza kuwa ili uchunguzi huo uweze kufanyika kwa uhuru Mhe. Rais ameamua kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake.

Waziri amesema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwa kuwa tuhuma  na malalamiko mengi ya awali yaliyojitokeza  dhidi yake yanajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi ambapo kwa sasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo  uchunguzi utakapokamilika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.