ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 23, 2017

RAIS JPM AMFUTA KAZI NAPE MNAUYE.


RAIS John Pombe Magufuli wa Tanzania leo Alkhamisi amefanya mabadiliko mengine katika Baraza la Mawaziri.
Taarifa ya Ikulu ya Tanzania imesema kuwa, katika mabadiliko hayo, Rais Magufuli amemteua Dk Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari,
Utamaduni Sanaa na Michezo, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na kada maarufu wa chama tawala cha CCM, Nape Nnuaye. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabadiliko mengine yaliyofanywa leo na Rais wa Tanzania ni kumteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Hata hivyo taarifa hiyo ya Ikulu ya Tanzania haikutaja hatima ya waziri wa zamani wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, bali imesema tu kuwa uteuzi huo unaaza mara moja na wateule hao wawili wataapishwa kesho Ijumaa mchana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania
Ikumbukwe kuwa jana Nape Nnauye alipokea ripoti ya tume aliyounda kwa ajili ya kuchunguza uvamizi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika majengo ya Clouds Media Group, uvamizi ambao umelalamikiwa vikali na duru mbalimbali hususan vyombo vya habari vya Tanzania.
Baada ya kupokea ripoti hiyo yenye mapendekezo kadhaa mazito, Nnauye alisema ataiwasilisha kwa wakubwa wake, Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania kwa ajili ya kuchukuliwa maamuzi. 

Miongoni mwa mapendekezo ya tume hiyo ni pamoja na Waziri Nape Nnauye awasilishe rasmi malalamiko ya tasnia ya habari dhidi ya Makonda.
Vyombo vya dola viwachunguze askari walioingia na bunduki kwenye kituo cha televisheni pamoja na kampuni ya Clouds Media kupitia upya miongozo, kanuni, sheria na taratibu ili kudhibiti watu wasiohusika kuingia kwenye chumba cha habari.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.