ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 12, 2017

MWENYEKITI CCM AKIONGOZA MKUTANO MKUU MAALUM MJINI DODOMA.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwahutubia wajumbe wapatao 2356,ambapo walipaswa kuwa wajumbe 2380 katika mkutano huo Mkuu Maalum wa CCM uliokuwa na lengo kuu la kufanya baadhi ya mabadiliko ndani ya Katiba ya chama hicho,ambapo mabadiliko hayo yamepitishwa kwa asilimia 100 na wajumbe hao waliohuhudria mkutano huo.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mambo mbalimbali mbele ya wajumbe waliohudhuria katika Mkutano Mkuu Maalum mjini Dodoma.

 Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu Maalum wa CCM wakishangilia kwa shangwe huku wakiwa na mabango yao yakionesha mikoa wanayoiwakilisha.

  Sehemu ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo pamoja na wageni waalikwa wakiwa tayari ukumbini.

  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano mkuu wa CCM, Mjini Dodoma

  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano huo.

   Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wastaafu wa Serikali na kichama walipowasili kwenye ukumbi wa mkutano na kukaribishwa na wajumbe.

 Mabalozi na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali  ndani na nje ya nchi wakiwa wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,mjini Dodoma.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.