ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 14, 2017

AUDIO:- MBUNGE WA NYAMAGANA ANUSURIKA KIFO, ASEMA MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU.

Watu watano akiwemo Mbunge wa Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula, mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi John Dotto na  wamenusurika kifo baada ya kupata ajali eneo la Dumila mkoani Morogoro, wakiwa safarini kutokea mjini Dodoma kuelekea Jijini Dar es salaam.

Mwandishi wa gazeti la Mwwananchi John Dotto ambaye alikuwa kwenye gari lililopata ajali alimokuwemo Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula.
Kwa mujibu wa mdogo wake Mbunge huyo anayejulikana kwa jina la Max, akizungumza na kipindi cha KAZI NA NGOMA toka radio Jembe Fm Mwanza, Max ambaye anamawasiliano ya karibu na msafara huo amesema kuwa alipata taarifa juu ya ajali hiyo jana majira ya saa nne usiku  na kuambiwa kwamba wako salama ingawa alipata shaka shaka baada ya kukosa mawasiliano na Mhe. Mbunge.

Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM)
"Nilipata faraja baada ya kuambiwa kuwa wote wako salama na kuisikia sauti ya Mabula ikizungumza na kusisitiza kwa vitu vilivyokuwa vikiendelea eneo la ajali" Alisema Max.

"Baadaye nilipata maelezo kuwa baadhi yao wamepata majereha, na kuambiwa kuwa wanaelekea Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwaajiili ya huduma ya uchunguzi na ikiwezekana matibabu" 
JIONI HII Gsengo wa Jembe Fm amezungumza na Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula baada ya kukabidhiwa simu yake na wananchi kwani ilianguka kwenye eneo la ajali naye anafunguka hivi BOFYA PLAY KUMSIKILIZA MBUNGE MABULA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.