Mazungumzo ya kupiga marufuku silaha za
nyuklia yameanza mjini New York Marekani bila ya kuwashirikisha wajumbe
kutoka Russia, Marekani, Ufaransa na Uingereza.
Shirika la habari la IRNA
limeripoti kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York kuanzia
leo Jumatatu hadi tarehe 31 mwezi huu yatakuwa mwenyeji wa mazungumzo
yanayohusu uandaaji wa mkataba unaopiga marufuku na kutaka kuangamziwa
kikamilifu silaha za nyuklia, mazungumzo ambayo yanafanyika bila ya
kushiriki wajumbe kutoka Russia, Marekani, Uingereza na Ufaransa ambazo
ni kati ya madola yanayomiliki nguvu za nyuklia duniani.
Kombora la nyuklia la Marekani. |
Uamuzi huo wa kuandaa rasimu ya mkataba
huo ulichukuliwa mwezi Disemba mwaka jana na Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa. Nchi zaidi ya 100 zimeunga mkono azimio linalounga mkono
kuandaliwa rasimu ya mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia, hata
hivyo Russia na nchi nyingine 35 wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepinga
azimio hilo.
Madola yanayomiliki silaha za nyuklia
duniani zikiwemo Russia na Marekakani zimepinga wazo hilo la kupasisha
mkataba unaozuia uundaji silaha za nyuklia.
Hii ni katika hali ambayo, madola
makubwa duniani yaani nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa zingali zimeazimia kumiliki maghala yao ya silaha
za nyuklia, licha ya kuwepo jitihada za kimataifa za kupunguza maghala
ya silaha za nyuklia khususan kuwepo mkataba unaopiga marufuku uenezaji
na usambazaji wa silaha hatari za nyuklia (NPT).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.