ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 13, 2017

HII AIBU...BASATA YAITAKA KAMATI YA MISS TANZANIA KUMKABIDHI MSHINDI GARI YAKE.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akionekana kumkabidhi gari mrembo huyo siku muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.
Ikiwa imepita zaidi ya miezi minne tangu shindano la Miss Tanzania 2016  lifanyike huko jijini Mwanza na taji lake kuchukuliwa na mrembo Diana Edward, bado mrembo huyo hajakabidhiwa zawadi yake ya gari na kiasi cha pesa Shilingi milioni mbili.
 

Hata hivyo katika siku ya mwisho wa shindano hilo, mrembo Diana alionekana akikabidhiwa gari aina ya Toyota IST, Ukumbini hapo kumbe ilikuwa danganya toto kwa watu wote waliofika katika shindano hilo ili waweze kuamini kuwa mrembo huyo kuwa kapewa gari.

Diana ambaye alikaa kwenye gari hiyo akiwa na furaha kubwa sana akimini kuwa ndio mchuma wake wa kwenda nao nyumbani kwao lakini mpaka leo mrembo huyo bado ni mtu wa kupanda daladala , Bajaj na Bodaboda.

Akizungumza na Ripota wetu, afisa habari wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Agnes Kimwanga amesema kuwa waliwaita kamati ya Miss Tanzania katika kikao cha tahmini na wao kukiri kuwa hawajampatia zawadi zake zote mshindi huyo pamoja na washiriki wengine  wanne.





“mara baada ya kujieleza katika kikao chetu cha Tathmini wakajitetea kuwa watatoa zawadi hizo tarehe 30 Aprili mwaka huu kwa kumpa Miss Tanzania 2016 zawadi yake ya gari na kiasi chake cha pesa Milioni mbili ambacho kimebaki” Amesema Agnes.

Akithibitisha hilo, Afisa habari wa Miss Tanzania, Haiden Ricco alikiri kutomlipa mrembo huyo stahiki zake zote ikiwepo gari.

"Ni kweli mrembo wetu hajawalipwa na sio yeye peke yake, hata wale warembo wengine wanne hawajalipwa pia" alisema Ricco.

Amesema kuwa fedha zilizobakia wanazodaiwa na warembo hao ni kiasi cha jumla ya shilingi milioni nane hivyo zote watalipwa kuanzia mwezi huo wanne.

Rico ametaja kuwa shindano lao kwa kutegmea wadhamini wamejipanga kuanzia mwezi ujao kuanza kuwalipa warembo hao kadri watakavyokuwa wanapata fedha kutoka kwa wadhamini na wadau wa shindano hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.