ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 19, 2017

GRACA MACHEL: SINA CHA KUWAFUNZA WAKE WA MARAIS

Dar es Salaam. Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Bibi Graca Machel amesema hawezi kuwafundisha wake wa marais kufanya anachofanya yeye katika kuhudumia jamii.

Graca amesema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam alipokuwa nchini kwa ajili ya Mpango wa Kuwainua Wanawake Afrika (WWA) aliosema kuwa wanawake wa Tanzania watanufaika nao.

 “Ni swali gumu kwangu, kwa sababu sina cha kuwafundisha wake wa marais, kila mtu anachagua namna ya kuleta tofauti katika jamii. Mimi nilichagua yangu na ndiyo hii,” amesema.

Hata hivyo, amesema hajioni kuwa ni mke wa rais, bali mwanamke aliyepata fursa na aliyeona upungufu katika nyanja mbalimbali za wanawake na kuamua kuzifanyia kazi.

“Kabla ya kuwa mke wa rais nilikuwa Waziri wa Elimu Msumbiji, tayari nilikuwa serikalini na niliona na kujifunza vitu vingi kuhusu elimu. Kwa hiyo hilo lilinipa mwanga na nilianzia hapo,” amesema.

Amesema kuwa mke wa rais siyo nafasi iliyonifanya awe alilivyo, bali alianza kujengwa hivyo kabla hata mume wake wa kwanza, Samora Machel hajafariki dunia.

Graca amedokeza kuwa hata alipokuwa msichana mdogo aliangalia mazingira aliyokuwa nayo na fursa zilizokuwapo ambazo zilimfungua macho na masikio na kupanga kuja kuzishughulikia ukubwani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.