ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 7, 2017

CHADEMA YATOA SALAMU ZA POLE KWA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE NA FAMILIA YAKE.

KUTOKA makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mkuu wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tumaini Makene, imetolewa taarifa yenye maneno ya Mwenyekiti Freeman Mbowe kwenye salamu za pole na Rambirambi kwa Mstaafu Jakaya Kikwete kwa msiba wa Mama yake mdogo Nuru Khalfan Kikwete uliotokea usiku wa kuamkia leo.

Akitoa salaam hizo kwa niaba ya Viongozi, Wanachama, Wapenzi na Wafuasi wa CHADEMA, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa familia ya Kikwete imepata pigo kubwa kuondokewa na moja ya nguzo muhimu katika familia na ukoo.

“Natoa pole za dhati kwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete na familia yake kwa kumpoteza Mama na Bibi katika wakati ambao walikuwa wakihitaji kuendelea kunufaika na matunda ya umri wake hasa hekima, busara na malezi“

“Wakati tukimuombea kwa mola marehemu Bi. Nuru alale mahali pema kwa amani, tunaomba pia Mwenyezi Mungu awapatie ujasiri na nguvu familia ya Kikwete kuukabili msiba huu, na awafanyie wepesi katika majonzi ya kuondokewa na mama” – Freeman Mbowe

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.