ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 29, 2017

BAHRAIN YAMFUNGA MIAKA 10 MBUNGE WA ZAMANI WA AL-WEFAQ.


Gazeti la al-Wasat limeripoti kuwa, Hassan Isa, mmoja wa viongozi wa chama cha Kiislamu cha al-Wefaq amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, kwa tuhuma bandia za 'kufadhili ugaidi'.
Mwanachuoni huyo ambaye pia alikuwa Mbunge wa chama cha al-Wefaq anatuhumiwa kuhusika katika hujuma iliyopelekea kuuawa maafisa wawili wa polisi na wengine kadhaa kujeruhiwa, madai ambayo amekuwa akiyakanusha vikali. 
Namna utawala wa Manama unavyotumia mkono wa chuma dhidi ya waandamanaji wasio na silaha nchini Bahrain
Wakati huohuo, mahakama ya Bahrain imewahukumu adhabu ya kifo Mohammed Ibrahim al-Tawq na Mohammed Radi Abdullah, wanaharakati na wakosoaji wakubwa wa serikali wa Manama. Kadhalika wanaharakati wengine watano wamehukumiwa adhabu ya kifo, ambapo wanne kati yao wamepokonywa uraia.
Haya yanajiri wiki mbili baada ya utawala wa wa ukoo wa Aal-Khalifa kuakhirisha tena kutolewa hukumu dhidi ya Sheikh Isa Qassim, mwanazuoni mashuhuri wa Bahrain hadi Mei 7 mwaka huu. 
Utawala wa kiukoo wa Bahrain unamtuhumu Sheikh Qassim kwamba amekuwa akieneza chuki za kimadhehebu miongoni mwa watu wa  nchi hiyo, kuchochea machafuko na kuhatarisha usalama wa taifa.
Ikumbukwe kuwa nchi kadhaa za Kiarabu hususan Saudi Arabia zimetuma wanajeshi wao nchini Bahrain kwa ajili ya kuwakandamiza raia wanaoandamana kwa amani kupigania haki zao za kimsingi kabisa kama vile haki ya kujichagulia wenyewe viongozi wao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.