ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 28, 2017

BAA LA NJAA NCHINI KENYA WATU MILIONI 3 WANAHITAJI MSAADA WA CHAKULA.


SHIRIKA la Msalaba Mwekundu limesema Kenya inahitajia msaada wa dharura wa chakula ili kunusuru maisha ya watu milioni 3 wanaokabiliwa na hatari ya kufa njaa kutokana na kushtadi ukame nchini humo.
Dakta Abbas Gullet, Katibu Mkuu wa shirika hilo amesema kuwa, hali ya kibinadamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki inazidi kuwa mbaya kutokana na kutonyesha mvua za kutosha, huku watoto wakiwa wahanga wakuu wa janga hilo.

Amesema kuwa, watoto zaidi ya laki 3 na 40 elfu walio chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo wa kiwango cha juu na kusisitiza kuwa, iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa, yumkini watapoteza maisha karibuni hivi. 

Athari hasi za ukame. Watoto wanakabiliwa na utapiamlo wa kiwango cha juu.
Mwezi uliopita, serikali ya Kenya ilitangaza ukame kuwa janga la kitaifa ambalo linahatarisha maisha ya watu, mifugo na hata wanyamapori.

Sambamba na tangazo hilo lililotolewa na Ofisi ya Rais Uhuru Kenyatta, Kenya ilizitaka taasisi za ndani na za kimataifa kuisaidia serikali ya Nairobi katika juhudi zake za kukabiliana na athari mbaya zilizosababishwa na ukame.

Hivi karibuni Shirika la Msalaba Mwekundu lilitahadharisha kwamba, watu zaidi ya milioni 11 katika nchi za Kenya, Ethiopia, Somalia na Sudan Kusini wamo katika hatari ya kufa njaa na wanahitaji kwa haraka msaada wa kibinadamu, kutokana na kukithiri kwa ukame.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.