ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 8, 2017

WAZIRI MKUU WA ZAMANI ASHINDA UCHAGUZI WA RAIS SOMALIA.


WAZIRI Mkuu wa zamani wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo ameshinda uchaguzi wa rais uliofanyika leo nchini humo chini ya ulinzi mkali.
Mohamed Abdullahi Farmajo ameshinda uchaguzi huo baada ya Hassan Sheikh Mohamud aliyekuwa akitetea kiti hicho kukubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Somalia uliowashirikisha wabunge.
Farmajo hakuweza kupata thuluthi mbili ya kura zilizohitajika kwa ajili ya kushinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 184 mkabala wa 97 za mpinzani wake, Hassan Sheikh Mohamud katika duru ya pili ya uchaguzi huo lakini ametangazwa mshindi baada ya rais anayeondika kujiondoa katika duru ya tatu.
Uchaguzi huo wa rais nchini Somalia umefanyika leo ukiwashirikisha wagombea 22 baada ya kuakhirishwa mara kadhaa.
Hassan Sheikh Mohamud, Rais anayeondoka wa Somalia.
Awali ilitazamiwa kuwa, mchuano mkubwa zaidi ungeshuhudiwa kati ya Rais wa sasa wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, Waziri wake Mkuu, Omar Abdirashid Ali Sharmarke na rais wa zamani wa Somalia Sharif Sheikh Ahmed.
Uchaguzi wa leo wa rais wa Somalia umefanyika katika hali ya utulivu wa kiwango fulani licha ya mashambulizi ya hapa na pale yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab.
Waziri Mkuu wa zamani ashinda uchaguzi wa rais Somalia


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.