ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 20, 2017

WANANCHI WA NZEGA MJINI WAZIDI KUNUFAIKA NA FEDHA ZA PROGRAMU YA WANANZENGO AIRTEL FURSA

Afisa Mikopo wa Nzega Urban Trust Fund, Bi. Elizabeth Mushi akiwa anatoa mafunzo ya mwisho kwa wajasiriamali na wafanyabiashara  waliofanikiwa kunufaika na Programu  wa WanaNzengo Airtel Fursa kwa awamu ya pii mara baada ya kupewa mikopo ya bei nafuu itakayowawezesha kukuza biashara zao. Mikopo hiyo inadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kusimamiwa  na Nzega Urban Trust Fund.
Wajasiriamali wa Nzega Mjini wakiwa wanaendelea kupokea mafunzo na maelekezo kutoka kwa Meneja wa Airtel Nzega, Bw. Abraham Mvella kuhusiana na namna sahihi ambayo watanufaika na fedha hizi kupitia Programu  hii ya WanaNzengo Airtel FURSA na namna ambavyo watakuwa wanarejesha marejesho ya mikopo ambayo wamechukua kutoka Airtel Tanzania.
Wanufaika wa Programu ya WanaNzengo Airtel Fursa awamu ya pili katika Picha ya Pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo ya ujasiriamali na kupokea fedha kwa njia ya Airtel Money.




Wananchi wa Nzega Mjini wazidi kunufaika na fedha za programu ya WanaNzengo Airtel FURSA

Baada ya mafanikio makubwa ya Programu  ya WanaNzengo Airtel FURSA uliozinduliwa Oktoba mwaka jana, na jumla ya shilingi milioni 20 kutolewa kama  mikopo isiyokuwa na masharti magumu kwa vikundi 20 vya wajasiriliamali takribani 100 wa mji wa Nzega,  tayari vikundi vingine 10 vyenye jumla ya watu 50 vimenufaika na fedha  kiasi cha shilingi million 10 ambazo zimetolewa katika awamu ya pili.

Akizungumzia mafanikio hayo mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe alisema  “Tangu tuzindue program hii miezi miwili iliyopita tayari program hii  imeendelea kuwa kivutio kikubwa cha uwezeshaji miongoni mwa wananchi wa kada mbalimbali ndani ya jimbo la Nzega mjini.  Program hii imekuwa kuvutio kwa wafanyabiashara, wajasiriamali pamoja an wafanyakazi mbalimbali. Tunapongeza kwa dhati  jitihada za pamoja baina ya Airtel Tanzania na Nzega Urban Trust Fund ambayo ni taasisi niliyoanzisha ili kuinua hali ya maisha ya wananchi wenzangu hapa Nzega Mjini.”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Nzega Urban Trust Fund, Bw. Felician Andrew alisema kuwa “Tunaishukuru sana Airtel Tanzania kupitia mpango wao wa Airtel FURSA kwani umeweza kuwafikia hadi watu wa kada ya chini kabisa hapa Nzega, mara ya kwanza wakati tunaanza programu hii tulitoa milioni 20 na sasa fedha zote zimeanza kurejeshwa na tumekusanya milioni 10 kwa njia ya Airte Money fedha ambazo ndizo tumezitumia tena kuzirudisha kwa wanafaika wapya kabisa kwa kutumia mfumo ule ule wa Airtel Money”

Naye Bi. Debora Mhamba mmoja wa wanufaika kutoka kikundi cha Ebenezer alisema kuwa  “mpango wetu ni kuwa kikundi chenye uwezo mkubwa wa kusimamia fedha zake na kupanua biashara zetu katika maeneo mengi zaidi  nje  ya Nzega, hivyo tutatumia vyema fedha hizi ili kufikia malengo yetu na kurudisha kwa wakati ili vikundi vingine viweze kunufaika na fedha hizi”

Kwa upande wake Meneja huduma za kijamii, Hawa Bayumi alisema tunafurahi kuona mradi unaendelea vyema na vikundi vingi vinaendelea kufikiwa zaidi, lengo letu ni kufika wasiriamali wengi zaidi ifikapo mwisho wa mwaka.  Natoa wito kwa wakazi wa Nzega mjini kuendelee kuitumia fursa hii vyema  ili kuimarisha mitaji na biashara zetu na hivyo kuleta chachu katika maendeleo ya jamii zetu na nchi kwa ujumla”

Makabidhiano haya ya fedha hizi yalifanyika katika Ofisi ya Nzega Urban Trust Fund hapaNzega Mjini na kushuhudiwa na kuhudhuriwa na Meneja wa Airtel Mji wa Nzega, Bw. Abraham Mvella pamoja na maofisa mbalimbali wa Ofisi ya Mbunge.

Zoezi hili la utoaji wa pesa lilifanyika baada ya kumaliza uhakiki wa vikundi zaidi ya 100 vilivyotuma maombi  na kufanyiwa uhakiki  na tathimini ya biashara zao  ambapo  vikundi kumi vikaibuka kidedea kuwa na  sifa zaidi ya vikundi vingine kuweza kunufaika na fedha za Programu hii.

Utoaji wa fedha za mikopo kwa awamu ya pili uliambatana na mafunzo ya jinsi ya kufanya marejesho ya fedha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.