ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 2, 2017

SUALA LA OKWI KUTUA LIGI YA UGANDA NI GERESHA TU AMEPAKI AKISUBIRI USAFIRI BASI LA SIMBA...!!HATUA ya mshambuliaji Emmanuel Okwi kuvunja mkataba na klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark, na kujiunga na klabu ya SC Villa ya Uganda inatajwa na wachunguzi wetu wa masuala ya soka kuwa ni geresha tu na kwamba ni kama anaitumia klabu hiyo kama kituo cha basi akisubiri safari yake kuelekea Msimbazi kujiunga na Klabu ya Simba ya Tanzania. 

Inasemekana Okwi anasubiri msimu mkuu wa usajili mwezi wa nane baada ya ligi kumalizika.

FUATILIA mazungumzo yafuatayo yaliyofanyika ndani ya Kipindi cha Sports Ripoti ya Jembe Fm kinachoruka kila siki usiku saa 3:00 hadi 4:00 chini ya mtangazaji Juma Ayoo na hapa alikuwa akizungumza na Hashim Mwesigwa kutoka Kampala nchini Uganda. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
 Zaidi ya hapo Okwi amejiunga na klabu yake ya zamani (SC Villa) kwa mkataba wa muda mfupi utakao muweka hadi mwishoni mwa msimu huu 2016/2017.

Nyota huyo wa zamani wa Simba aliachana na SC Villa mwaka 2010 na kujiunga na Wekundu wa Msimbazi’ baada ya kuisaidia Jogoos kutwaa taji la Uganda mwaka 2009.

Mshambuliaji huyo mahiri wa Uganda amesema atahakikisha anaisaidia Villa iliyomkuza kufanya kweli.

“Dili tayari limekamilika,” Ivan Kakembo CEO wa SC Villa aliuambia mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.