ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 3, 2017

• POLISI WAKAMATA MASHAMBA MAWILI YA BHANGI YENYE UKUBWA WA EKARI 4, WILAYANI SENGEREMA.


TAREHE 01.02.2017 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA BUHINDI ULIPO KIJIJI CHA ILYAMCHELE TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA PAMOJA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WA SERIKALI YA BUHINDI WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA EKARI MBILI NA NUSU AMBALO LILIKUWA NDANI YA HIFADHI HIYO.

POLISI WALIPOKEA TAARIFA ZA UWEPO WA SHAMBA HILO LA BHANGI KUTOKA KWA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU HUO, NA KWAMBA WANANCHI AMBAO WANAOISHI KARIBU NA MSITU NDIO WALIOPANDA BHANGI HIYO KATIKA ENEO HILO NA PINDI WANAPOKATAZWA WAACHE TABIA HIYO WAMEKUWA WAKIKAIDI NA KUWATISHIA KUWAPIGA KWA MAWE MAAFISA WA HIFADHI HIYO. ASKARI WALIKWENDA PAMOJA NA MAAFISA HAO HADI ENEO LA HIFADHI YA MSITU NA KUKUTA ENEO LA EKARI MBILI NA NUSU LIKIWA LIMEOTESHWA BHANGI, ASKARI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA HIFADHI YA MSITU WALIFANIKIWA KUTEKETEZA SHAMBA HILO LA BHANGI LILILOKUWA NA JUMLA YA IDADI YA MICHE 7300 YA BHANGI. POLISI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI ILI KUWEZA KUWABAINI WATU AMBAO WALIHUSIKA NA KUOTESHA BHANGI KATIKA ENEO LA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA BUHINDI.

AIDHA KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE 02.02.2017 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KAFUNZO KILICHOPO WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA,   ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA MKORO MSAMI MIAKA 74, MKAZI WA KIJIJI CHA MAFUNZO, KWA KOSA LA KUOTESHA MICHE 84 YA BHANGI KWENYE SHAMBA LENYE UKUBWA WA EKARI MOJA NA NUSU, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA MTU KATIKA KIJIJI TAJWA HAPO JUU ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO CHA BHANGI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI JUU YA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA PAMOJA NA SHAMBA LAKE NA KUANZA ZOEZI LA  KUNG’OA MICHE YOTE YA BHANGI KATIKA SHAMBA HILO KISHA KUITEKETEZA KWA MOTO.

MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA ASKARI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIAKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA  NA MISAKO KATIKA MAENEO YOTE ILI KUWEZA KUWAKAMATA NA KUWADHIBITI WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI.


KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI, ILI LIWEZE KUWAKAMATA NA KUDHIBITI WATU WOTE AMBAO WANAJIHUSISHA NA KILIMO HARAMU CHA BHANGI NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.