ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 27, 2017

MWANA WA MUHAMMAD ALI ATIWA MBARONI KWA KUWA NA JINA LA KIISLAMU.


Mwana wa nguli wa masumbwi duniani marehemu Muhammad Ali, alikumbwa na adhaa baada ya kutiwa mbaroni katika uwanja wa ndege wa jimbo la Florida kwa kuwa na jina la Kiislamu.
Muhammad Ali Junior, mmoja wa watoto wa marehemu Muhammad Ali, alitiwa mbaroni katika uwanja wa ndege wa jimbo la Florida wakati alipokuwa akirejea kutoka nchini Jamaica kuingia Marekani. Habari zaidi zinasema kuwa, baada ya kutiwa mbaroni mwana huyo wa Muhammad Ali alihojiwa kwa masaa mawili.

Marehemu Muhammad Ali enzi za uhai wake akiwa na mke wake Khalilah Camacho Ali.
Muhammad Ali Junior alizaliwa katika mji wa Philadelphia katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani huku akiwa na pasi ya kusafiria ya nchi hiyo. Junior anaishi nchini Jamaica pamoja na mama yake, Khalilah Camacho Ali. Wakili wa mwana huyo wa Muhammad Ali, kwa jina la Chris Manshny amesema kuwa kijana huyo wa mwanamasumbwi mashuhuri duniani na mama yake walitiwa mbaroni katika uwanja huo wa ndege wa Florida mwezi huu kutokana na kuwa na majina ya Kiarabu.
Uwanja wa ndege wa Florida wakati mwana huyo wa Muhammad Ali alipotiwa mbaroni.
 Kwa mujibu wa wakili huyo, Bi, Khalilah Camacho Ali na mwanaye waliachiliwa, mara baada ya kuonyesha picha inayomuonyesha yeye akiwa na marehemu mume wake huku wakiwa tayari wamehojiwa kwa muda usiopungua masaa mawili. Tangu Rais Donald Trump wa Marekani aliposaini marufuku ya kuzuiwa raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia nchini  humo, Waislamu wamekuwa wakikumbwa na madhila mbalimbali ndani ya taifa hilo linalojinadi kuwa mtetezi wa haki za binaadamu duniani. Hii ni katika hali ambayo mahakama kadhaa za nchi hiyo zimetaka kutupiliwa mbali marufuku hiyo ya Rais Trump.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.