ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 8, 2017

MAUAJI YA SILAHA ZA MOTO YAONGEZEKA MAREKANI, WATU 58 WAUAWA KATIKA SIKU 2.

KITUO cha takwimu za ufyatuaji risasi nchini Marekani kimetangaza kuwa, kwa akali watu 58 wameuawa kwa kupigwa risasi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na kituo hicho imesema kuwa watu hao wameuawa katika matukio 149 ya ufyatuaji risasi katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita nchini humo. Kadhalika ripoti hiyo imesema kuwa katika matukio hayo watu wengine 89 wamejeruhiwa. Kabla ya hapo kuliripotiwa ongezeko la vitendo vya mashambulizi ya silaha za moto katika majimbo ya Florida, Ohio na Louisiana.
Silaha za moto nchini Marekani zikiuzwa hadharani
Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha takwimu za ufyatuaji risasi nchini Marekani, kuanzia mwanzo wa mwaka huu 2017 hadi tarehe sita ya mwezi huu, jumla ya matukio 886 ya hujuma za ufyatuaji risasi yameripotiwa nchini Marekani ambapo watu 568 wameuawa na wengine 2971 kujeruhiwa, takwimu ambazo zinaonyesha ongezeko kubwa la mauaji ya silaha za moto nchini humo. Itafahamika kuwa, kila mwaka maelfu ya watu huuawa na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na silaha hizo katika meneo tofauti ya nchi hiyo inayojinadi kuwa polisi wa dunia. 
Maelfu ya wanachuo mjini New York wakiandamana kupinga marufuku ya Rais Trump dhidi ya Waislamu
Katika hatua nyingine maelfu ya wanafunzi wa chuo kikuu mjini New York wamemiminika mabarabarani kupinga siasa za Rais Donald Trump wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo jana wanachuo hao waligoma kuingia madasani na badala yake wakashiriki katika maandamano makubwa ya kupinga marufuku ya kuwazuia raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia nchini humo.
Bi.  Betsy DeVos kuwa Waziri wa Elimu wa Marekani
Kadhalika wanafunzi hao wamekosoa vikali hatua ya rais huyo kumteua Bi, Betsy DeVos kuwa Waziri wa Elimu nchini humo na kwamba mwanamke huyo hana uzoefu wowote wa kusimamia masuala ya elimu nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.