ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 1, 2017

KAYA 16,485 (KUMI NA SITA ELFU MIANNE THEMANINI NA TANO)ZANUFAIKA NA TASAF WILAYA YA SENGEREMA KATIKA ALIMASHAURI YA SENGEREMA NA BUCHOZA

HAYO yamesemwa nae Mratibu wa Tasaf wilaya ya Sengerema  bwana Malisa Maxmilian Nduga wakati wa zoezi la ugawazi ruzuka wa kaya maskini lililofanyika katika kijiji cha Namililo kata ya Kasungamile wilayani humo akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Maxmilian amesema katika malipo ya january na february 2017,tasaf imetoa ruzuka ya sh millioni 600na 89 elfu kwa kaya maskini.

Akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa uchukuaji ruzuku kwa kaya isiyo kuwa na mama Maxmilian amesema mtu yeyote msimamizi wa kaya anaruhusiwa kuchukuwa ruzuku endapo serikali ya kijiji ikishakudhibitisha na endapo amefariki kuna utaratibu wa kubadilisha msimamizi

BOFYA PLAY KUMSIKILIZA Mratibu wa Tasaf

Akizungumza na wananchi hao afisa maendeleo alimashauri ya wilaya ya sengerema Bwana Bushaija amewataka kuzitumia fedha hizo kwa maendeleo kwa kuanzisha miradi midogo na kwawanao pata ruzuku kupitia watoto wanaosoma kuhakikisha wamapelekwa shule.

Kwaupande wake afisa elimu sekondari bwana Godwin Barongo amesema kuwa watoto walioandikishwa kwenda shule wote waende shulena endapo mtoto hatakwenda shule pesa ya ruzuku itapugua na kuongeza kuwa pesa hizo zisaidie kuwanunulia mavazi ikiwemo sale za shule

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo mjumbe wa serikali ya kijiji Bi Debora Clifod amesema changamoto ni kwa walengwa wasiofika siku ya utoaji ruzuku kutokana na dharula mbalimbali pesa zao kurudisha na mwezi unaofuata hawapatiwi

BOFYA PLAY KUMSIKILIZA Debora Clifod

Akijibu kuhusu changamoto mratibu wa tasaf alimashauri ya Sengerema amesema kuwa fedha zote ambazo hazijalipwa katika muda husika yanarudi katika kipindi cha malipo yanayofuata ingawa amekili kuwa siku awali kulikuwa na changamoto katika utendaji kwasasa changamoto hiyo imeshakwisha.

Bi Salome Andrea na bwana Emanueli Masanja ni wadau wa ruzuku  kwa upande wake bi Salome amesema kuwa tangu amepata ruzuku amefanikiwa kununua mifugo,mavazi ya watoto na chakula.Akiishukuru tasafu Emanuel Masanja amesema kuwa amefanikiwa kujenga nyumba imara na kuwapeleka watoto shule na kuanza ufugaji

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.