ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 8, 2017

GEITA :KUIMARISHA KILIMO CHA PAMBA

Mkuu wa mkoa wa Geita,Meja Jenerali Ezekiel Kyunga,akitfungua kikao cha wadau wa pamba Mkoani Humo.

Wajumbe wakifatilia kwa makini kikao Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe Nicas Mayala 

Wajumbe wakiendelea na majadiliano


Wakuu wa wilaya Mkoani Geita wakifatilia kikao.

Afisa kilimo wilaya ya Bukombe Joseph Machibya akitoa maelezo namna ambavyo wameweza kupiga hatua kwenye kilimo cha pamba.
PICHA NA Joel maduka
Imeandaliwa na www.madukaonline.blogspot.com

SERIKALI mkoani Geita ,imesema kuwa itahakikisha inaboresha zao la pamba kwa kutumia viadudu ambavyo  vitasaidia kunusuru pamba kwenye maeneo ya vijijini ambako wakulima wengi wanaendelea kulima.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la Pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Mkoa na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali  kutoka Wilaya zote za mkoa wa Geita wakiwemo Maafisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika pamoja na Wakuu wa Bodi ya Pamba kanda ya ziwa,

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,amesema  kuwa pamoja na hali ya changamoto ya ukame  na mvua kunyesha kwa uchache bado  wakulima wameitikia wito na kulima  hali ambayo kwa sasa inatia matumaini kutokana na pamba kuoto vizuri vijijini.

“Huko vijijini wamaenza kulalamika kutokana na upungufu wa viuadudu sasa na sisi hapa lazima tupate uvumbuzi kwamba hili tatizo la viuadudu tunalipatia majibu sahihi ambayo yatawasaidia wakulima wetu kule vijijini, wakulima wameitikia vizuri pamoja na hali hii ya mvua ambazo sio kamilifu, mvua ni chache, mvua ni haba lakini wakulima wameitikia” alibainisha mh kyunga

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe akiwemo Emily Kasagara  Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Geita na Safari Mayala Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe wameelezea  changamoto dhidi ya zao la pamba na  kusema   kuwa.

“Kuna changamoto mbalimbali zilizojitokeza kuhusiana na zao hli la pamba, moja ni kuwa wakulima wengi walielekeza nguvu zaidi kwenye mazao ya chakula kipindi mvua zilipoanza kunyesha na badala ya zao la pamba kwa hiyo ndio maana hata katika taarifa yetu kile kilimo cha pamba kiliextend mpaka mwezi Januari kwa sababu mvua zilipoanza kunyesha tu wakawa wamerash kulima mazao ya chakula lakini baadae sasa wakalima zao letu la pamba ambalo limeenda  mpaka Januari” alisema

Aidha katika  msimu wa mwaka 2016-2017 Mkoa ulilenga kulima jumla ya tani elfu sitini na saba na mbili (67,002) zilizotarajiwa kutoa mavuno ya tani elfu tisini na tatu mia nne thelathini na saba (93,437)  lakini changamoto  ya mvua za vuli kutonyesha vizuri katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Geita imeweza kusababisha malengo hayo kutokufikiwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.