ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 19, 2017

PROF MUHONGO AMEWATEMBELEA WAHANGA 15 WA TUKIO LA KUFUKIWA NA KIFUSI NYARUGUSU NA KUTOA MAAGIZO KWA KAMISHINA WA MADINI.

Waziri wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo wakati alipokwenda kuwatembelea wahanga wa mgodi wa RZ UNION ulijifukia mwezi wa kwanza mwaka huu kwenye kijiji cha mawemeru Kata ya Nyarugusu Wilaya  na Mkoa wa Geita.

Waziri wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo akisalimiana na mmoja kati ya wafanyakazi wa mgodi wa RZ UNION

Waziri wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo na msemaji na mwanasheria wa Mgodi wa RZ UNION ,Frances Kiganga wakati alipotembelea mgodi huo.


Waziri wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo akisalimiana na meneja wa mgodi huo ,Bw Gexiu Liu.

Waziri wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo akizungumza na baadhi ya wahanga wa tukio la kufukiwa na kifusi.

Waziri wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo,akiteta jambo na mkuu wa Mkoa wa Geita meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga

mkuu wa Mkoa wa Geita meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga akimkaribisha waziri wa nishati na madini kuzungumza na wahanga wa tukio hilo.


Baadhi ya wahanga na wasio wahanga wakifatilia kile ambacho kilikuwa kikiendelea 

Msemaji na Mwanasheria wa Mgodi huo,Frances Kiganga akiwakilisha taarifa kwa waziri wa nishati na madini.

Anset Masanja akimwelezea waziri wa nishati na madini namna ambavyo hali ilikuwa siku nne ambazo walikuwa wamefukiwa na kifusi.


Mbunge wa Jimbo la Busanda,Lorencia Bukwimba akimweleza waziri wa nishati na madini namna ambavyo wachimbaji wamekuwa wakikutana na wakati mgumu katika shughuli zao za uchimbaji na kumwomba aweze kuwasaidia wananchi eneo la Stamico ambalo limekuwa likililiwa na wachimbaji wadogo.

Waziri wa Nishati na madini,Professa Muhongo akimweleza Mbunge Bukwimba namna ambavyo wizara imejipanga kuwasaidia wachimbaji wadogo.


Waziri wa Nishati na madini,Professa Muhongo akizungukia maeneo ya mgodi wa RZ.


Waziri wa Nishati na madini,Professa Muhongo,Akipatiwa maelezo na msemaji wa mgodi wa RZ kwenye eneo ambalo waliwaokolea ndugu ambao walifukiwa na kifusi.

Moja kati ya wahanga wa tukio hilo akionesha ramani ya shimo ambalo lilijifukia kwa waziri wa nishati na madini,Mh Prof Sospeter Muhongo.

Na Joel Maduka wa
 www.madukaonlin.blogspot.com

WAZIRI wa nishati na madini ,Professa Sospeter Muhongo,amemwagiza Kamishina wa madini kanda ya ziwa kutembelea migodi yote na kuikagua ili kujua hali ilivyo na kuakikisha wanatoa mashariti katika migodi yote mikubwa,ya kati na midogo.

 Hayo ameyasema wakati  alipowatembelea wachimbaji kumi na tano ambao walifukiwa na kifusi kwenye mgodi wa RZ union uliopo kwenye kijiji cha mawemeru Kata ya Nyarugusu wilaya na Mkoa wa Geita.

Prof,Muhongo amemwagiza kamishina wa madini kuakikisha anafanya ukaguzi na kutembelea migodi yote na kwamba kufikia tarehe 16 ya mwezi wa tatu awe ametoa taarifa ya hali ilivyo kwenye migodi ambayo hatakuwa ametembelea.

“Kamishina nimekwisha waelekeza tembeleeni Migodi yote mkague na kwasababu watu wanaendelea kuchimba kama nyie ni wachache tuongezeni nguvu kutoka wizarani,kutoka stamiko,siorojiko au chuo kikuu leo ni tarehe 17 hadi kufikia 16 mwezi ujao nipewe ripoti ya ukaguzi”Alisisitiza Prof Muhongo.

Kamishina  Msaidizi wa madini  kanda ya ziwa victoria magharibi Yahaya Samamba ,amemweleza waziri wa nishati na madini sababu zilizopelekea kuanguka ni kutokana na kuzidiwa kwa udongo uliokuwa juu pamoja na kuwa ni mgodi wa muda mrefu hivyo timba zilikuwa zimekwisha anza kuoza na kwamba hatua ambazo zimechukuliwa hadi sasa ni mgodi kufungwa hadi yale maelekezo waliyopatiwa yatakapo kuwa yamekamilika.

“Uchunguzi uliofanyika umeonyesha kuwa mgodi huu umeanguka kutokana na kuzidiwa  na udongo laini juu pia mwamba laini ulioza kiasi cha takribani mita 15 kutoka usawa wa ardhi lakini pia sambamba na hilo mgodi huu una muda mrefu zaidi ya miaka mitatu kwa hiyo zile sapoti kwa maana ya timba zilikuwa zimekwisha hanza kuoza na tulikuwa tumekwisha wapo maelekezo wakati wakiwa kwenye marekebisho ya kuweka chuma ndio ajali hii iliweza kutokea kazi inayoendelea hivi sasa ni kutoa maji kwenye shimo ili kuakikisha mazingira yanakuwa mazuri ili kufanya yale ambayo yameagizwa na kamishina wa madini”Alisema Samamba.

Kwa upande wake msemaji wa mgodi huo na mwanasheria,Francis Kiganga ,amemwomba Waziri wa nishati na madini kutia sahini ya hati ya uhamishaji miliki kwa maana pande zote mbili wamekubaliana kwa muuzaji abaki na asilimia 15 na mnunuzi ahamishiwe asilimia 85.

Hata hivyo ombi hilo alikukubaliwa na waziri wa nishati na madini hadi pale mgodi huo utakapokuwa umetimiza mashariti ambayo wamepatiwa.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi,amemweleza waziri Muhongo kuwa  wamefatilia kuakikisha vijana wanapatiwa mikataba ya kudumu .
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wenzake ambao walinusurika kwenye ajali hiyo Ansenti Masanja amemshukuru waziri Muhongo kwa kuwatembelea na kuja kuwajulia hali zao ikiwa ni pamoja na  kuwapa pole.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.