Katika uwanja wa ndege wa Mwanza kuna malumbando baina ya wadau wafanyakazi wa ndege hiyo sanjari na abiria ambao wanataka majibu ya haraka kujua hatma ya safari yao.
Ndege hiyo iliruka kwa takribani dakika 20 na kisha kulazimika kutua kwa dharura hali iliyozua taharuki kwa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Tayari Ofisa Habari wa ATCL Lily Fungamtama amekiri kutokea kwa tatizo hilo na kusema kuwa ndege hiyo iliruka lakini ililazimika kutua kutokana na tatizo la kiufundi.
"Baada ya Rubani kuona tatizo hilo, alitoa taarika kwa mafundi ambao walirekebisha tatizo na ndege hiyo sasa ipo kazini kama kawaida"
Naye kaimu wa Uwanja wa ndege wa Mwanza David Motovolwa alikiri kuwepo kwa tatizo hilo huku akidai kwamba ndege hiyo ilishindwa kuruka kutokana na hitilafu kwenye injini.
ZAIDI sikiliza Jembe Fm
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.