ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 17, 2017

WACHEZAJI KLINIKI YA ARS WAASWA KUJITUMA.


Wachezaji kliniki ya ARS waaswa kujituma

Wachezaji wanaoshirki kliniki ya mpira wa miguu ya  Airtel Rising Stars wameaswa kujituma ili kufanikisha malengo yao ya kuwa wachezaji bora na  wakulipwa nchini.

Akizungumzia kuhusu siku ya pili ya mafunzo hayo, Kocha Mkuu wa Timu ya  Serengeti Boys, Bakari Shime  alisema kuwa mafunzo ya leo yamelenga kumiliki mpira, kuomba na kutoa pasi. Shime aliongeza kwa ku kusema ukitaka kucheza kwa mafanikio ni lazima  mchezaji awe na uwezo wa kumiliki mpira na ili kufanikisha hilo ni lazima mchezaji awe na stamina nzuri.

Kliniki ya Airtel Rising Stars ambayo ilizinduliwa jana Jumatatu inaendelea mpaka Jumamosi ambapo wachezaji bora watachaguliwa kujiunga na timu ya vijana ya Serengeti Boys pamoja na Kilimanjaro Queens

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.