ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 22, 2017

VIGOGO WA CHADEMA JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI WAMKATAA MBUNGE WAJIHUDHULU NAFASI ZAO CHA CHAMA

VIGOGO: Waliokuwa viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Ikungi na Jimbo la Singida Mashariki walioamua kujihudhulu nafasi zao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) Wilaya hiyo, Anna Benedicto (kushoto) na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Wilaya, Theotimi Mughanga (kulia) wakisubilia kuongea na waandishi wa habari juu ya uamuzi wao. Picha Na Peter Fabian 

Na PETER KATULANDA Aliyekuwa SINGIDA.

VIONGOZI  wawili wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wajiuzulu nafasi zao kwa madai ya kuchoshwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) kwa tabia yake ya kuwahamasisha wananchi kutochangia shughuli za maendeleo.

Hatua hii imetafasiriwa na wananchi wengi kuwa ni pigo kwa Mbunge na Chama hicho kuendelea na siasa ambazo hazina tija kwao bali kwa masilahi ya wachache ambao wamepelekea Jimbo hilo kupaki nyuma kimaendeleo nap engine ndiyo mwanzo na mwisho wa Chama hicho katika Wilaya hiyo kutokana na wananchi kutoshirikia shughuli za maendeleo na wao kukosa huduma bora za kijamii.

Wakizungumza na waandishi wa habari juzi Mjini Ikungi, Theotimi Mughanga aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya na Jimbo hilo na Anna Benedicto aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama hicho (BAWACHA) alieleza kuwa uamuzi huo wa kuachia ngazi ni uamuzi usiokuwa na shinikizo la mtu bali kwa ihali yao.

Mughanga alisema kwamba wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015 walipita kwa wananchi wakiomba wakichague chama hicho pamoja na mgombea Ubunge Lissu  ili kupata ridhaa ya kuwatumikia na wakawachagua lakini imekuwa tofauti kwa Mbunge huyo kupora madaraka ya viongozi wa Chama na kupandikiza mbegu mbaya ya chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali na vyama vingine vya siasa.

“Haonekani Jimboni lakini pia anapokuja hufanya mikutano ya kuhamasisdha wananchi kutoshiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuchangia, Pia amekuwa akiwatolea lugha isiyo na star viongozi na madiwani kwa madai wasifanye kitu bila yeye kuamua jambo ambalo tumeamua kumpinga na ili kudhihilisha tumemchoka tumeamua kuachia ngazi,”alisema.

Aidha aliyataja mbambo matano yaliyowafanya kuchukua uamuzi huo kuwa ni kuminywa kwa demokrasia kulikopitiliza ndani ya Jimbo la Singida Mashariki, Viongozi wa Chama (CHADEMA) kutothaminiwa na kuongozwa kidikteta na Mbunge Lissu, kutotekelezwa kwa ahadi mbalimbali za Mbunge alizozitoa kwa wananchi wakati wa Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na 2015.

Katibu huyo pia alienda mbali zaidi kwa madai kuwa, dhamira inawasuta kwa kushindwa kuwatumikia wananchi ikiwemo kuwaongoza kwa kutowabagua jambo ambalo wameshindwa kutokana na Mbunge huyo kuliendeleza kwa kupoka madaraka ya viongoziwa Chama yeye na Madiwani.

“Amekuwa akizuia wananchi kushirikiana na serikali katika kuboresha miundombinu ya Afya, Maji, Kilimo, Ufugaji, Elimu ambapo amekuwa akiwazuia kuchangia hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara, vyoo vya shule na shughuli zingine za kijamii kwa madai hayo yatafanywa na serikali nay eye kama Mbunge atapiga kelele jambo lililopelekea Wilaya na Jimbo kubaki nyuma kimaendeleo.
Naye Mwenyekiti wa BAWACHA  (Wilaya) Anna Benedicto  aliyeamua kuachia ngazi  alimshutumu Mbunge Lissu kutumia fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo kwa ulaghai mkubwa kwa kuandaa vikundi hewa na kuvigawia fedha kinyume na utaratibu pamoja na kutotekeleza miradi ambayo ingesaidia kukamilishwa na kutoa huduma kwa jamii.

“Tumepoteza mwelekeo kwa wananchi waliotuamini na kukichagua Chama kuwawakilisha wananchi ikiwa ni pamoja na kuwezesha wanapiga hatua ya maendeleo ikiwemo kupata huduma bora za kijamii lakini leo Jimbo la Singida Mashariki ndilo linashika mkia katika Mkoa wa Singida kwa kila kitu iweni kilimo, hutoaji huduma za jamii na kuwaungabni wananchi wake kuwa wamoja,”alisema.

Benedicto alimpongeza Rais Dk John Magufuli kwa hatua zake za kurejesha imani ya serikali kwa wananchi kwa kuhakikisha anapambana na vitendo vya rushwa, ufisadi, uwajibikaji wa watumishi wa umma, nidhamu kwa viongozi na watumishi pamoja na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM ikiwemo Elimu bure na kuwaacha viongozi wa Chadema wakiweweseka.

“Leo tulichokuwa tunakipigania tukiwa CHADEMA ndicho anakifanya Rais Dk Magufuli hivyo hoja ya Upinzani imekufa na sasa wameanzisha hoja  za sukari, njaa, mikutano ya hadhara ambazo kimsingi haziwasaidii wananchi bali ni kutaka kutumia fursa hiyo kuwachochea waichukie serikali ambayo kila kukicha inahangaika na maisha ya wananchi walio masikini,”alisema.

Benedicto alitoa wito kwa wafuasi na wanachama wa CHADEMA Wilaya ya Ikungi na Jimbo la Singida Mashariki kupima mwelekeo wa Mbunge Lissu ambaye ameshindwa kuwasaidia kwa kisingizio cha majukumu ya kitaifa na kutorudi hata kuwahamasisha kwa ajili ya maendeleo na Madiwani pia kuongozwa kidikteta na Mbunge ili kuwezesha kutowarejesha wagombea wa Chadema mwaka 2020 ikiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.