ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 18, 2017

WANAHABARI WAIPELEKA MAHAKAMANI SHERIA YA HABARI.

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, kifafanua jambo mbele ya wandishi wa habari mkoani Mwanza mara baada ya kutoka mahakamani kufungua kesi dhidi ya Sheria ya Habari, kulia ni Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji.
Nje ya Mahakama kabla ya kufunguliwa kwa esi hiyo tulipata nafasi ya kuzungumza na Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha wandishi wa habari wanaopiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu nchini Tanzania hapa anafunguka ni kipi kinachofanyika. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Mwanaharakati Jenerali Ulimwengu naye ameungana na wadau wenzake wa tasnia ya habari mahakamani hapa.

Na  Zephania Mandia
GSENGO BLOG
MWANZA.

Umoja wa klabu ya za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC na kampuni ya Hali halisi Publishers Limited leo wamefungua kesi ya katika Mahakama  Kuu ya Tanzania Mwanza wakidai kuwa sheria ya huduma ya vyombo vya habari 2016 inakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 5,2016.katika kufungua kesi hiyo,timu ya wanasheria Fulgence Massawe, Edwin Hans, Jenerali Ulimwengu, Jebra Kambole, Frances Stolla, Mpole Mpoki. hawa wote wanaziwakilisha taasisi hizo katika mahakama kuu.


Walalamikaji wanadai kuwa baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vinakandamiza uhuru wa kujieleza vinakiuka ibara ya 18 ya katiba ya nchi.


Ibara ya 18 inatoa haki kwa kila mtu kuwa na uhuru wa maoni na fikra zake,kutafuta,kupokea habari bila ya kujali mipaka ya nchi, uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano hayo.


Katiba pia inatoa haki kwakila mwananchi kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu maswaala muhimu kwa jamii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.