ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 31, 2017

TRA WATOA SEMINA KWA WASIOSIKIA.

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa semina kwa walemavu wasiosikia 56 Mkoani hapa ili kupanua wigo wa ukusanyaji wa kodi za Serikali na kuwahamasisha kuwa na ujasiri wa kuchangamkia fursa zilizopo ili kujiongezea kipato.

Semina ilitolewa mwishoni mwa wiki baada ya kundi hilo kuwa limesahaurika kuhusiana na Elimu ya ulipaji kodi wakati baadhi yao wakiwa wanafanya biashara mbalimbali kwenye jamii.

Akizungumza na walemavu hao Meneja wa TRA Ernest Dundee amesema fursa ni nyingi za kufanya na kwamba wanayo nafasi ya kuchangia kwenye maendeleo ya nchi hata kama ni kidogo.

“Kundi hili  tulilisahau kwa muda  mrefu kulishirkisha katika masuala ya kodi ukiacha siku ya leo  hivi sasa mnaweza kufika muda wowote na kupata semina ya kodi   na kuelimika”amesema  Dundee.

Akitoa mada ya ujasiriamali na kodi, Ofisa mwanadamizi wa huduma na Elimu ya kodi wa TRA Mkoa wa Mwanza Lutufyo Mtafya amesema wanatakiwa  kuwa na dira ya  kushirkiana  itakayowaongoza katika biashara.

Amesema unapoanzisha shughuli ya kibiashara ifahamike kuwa kuna taasisi zinazoweza kusimamia kama TRA kwa ajili ya ukusanayaji wa mapato ya serikali hivyo wanatakiwa kuwa na TIN pamoja na leseni kwa mujibu wa sheria.

“Unapofanya biashara ujue unajukumu la kutoa risti kama leseni inavyotaka kwa mteja  ili tusipoteze mapato ya nchi kwa ajili ya maendeleo yetu, hizi barabara tunazopita ni kodi,madawa hospitalini ni kodi kwa hiyo inatupasa tufate sheria na taratibu za kibiashara”amesema Mtafya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.