ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 27, 2017

DECI NYINGINE MBILI ZANASWA MKOANI MWANZA, WAMEPIGA HELA YA HATARI KWA WANANCHI.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 26.01.2017

·         TAHADHARI YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI JUU YA UWEPO WA VIKUNDI VYA WAHALIFU WANAOIBIA WANANCHI FEDHA ZAO KWA KUWASHAWISHI KUJIUNGA NA BIASHARA YA UPATU ( KUWEKEZA FEDHA KIDOGO NA BAADAE KULIPWA FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI BILA KUFANYA KAZI YEYOTE)  KAMA ILIVYOKUWA DECI .

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA DCP: AHMED MSANGI ANATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIHADHARI/KUJIEPUSHA NA WATU/VIKUNDI VYA WATU AMBAO NI WAHALIFU WALIOKUSUDIA KUJIPATIA FEDHA NYINGI TOKA KWA WANANCHI KWA KUWADANGANYA/ KUWARUBUNI WAJIUNGE NA BIASHARA YA UPATU AMBAPO WANANCHI HAO HUSHAWISHIWA KUWEKEZA FEDHA KIDOGO KWA MUDA MFUPI KATIKA VIKUNDI HIVYO NA BAADA YA HAPO WANAAHIDIWA KULIPWA FEDHA NYINGI ZAIDI YA ZILE WALIZO WEKEZA BILA KUFANYA KAZI YEYOTE. BIASHARA HIYO INATAMBULIKA KWA JINA LISILO RASMI LA KUPANDA MBEGU NA KUVUNA.

HIVI KARIBUNI KUMEJITOKEZA WIMBI KUBWA LA VIKUNDI VYA NAMNA HIYO HAPA JIJI MWANZA NA TAYARI WANANCHI WENGI WAMEIBIWA FEDHA ZAO. KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA UHALIFU WA AINA HII JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZISHA NA LINAENDELEA NA MISAKO MAENEO MBALIBALI YA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWA LENGO LA KUBAINI NA KUWAKAMATA WATU/VIKUNDI VINAVYOFANYA UHALIFU HUO. (UPATU)

AIDHA KAMANDA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU VIKUNDI VIFUATAVYO AMBAVYO UPELELEZI UMEONESHA KUWA VINAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU AMBAVYO NI; KIKUNDI KINACHOJULIKANA KWA JINA LA AQ POWER CLUB KINACHOMILIKIWA  NA HAPPY ALOYCE MBUYA MIAKA 35, MCHAGA , MKAZI MTAA WA ILIEMELA ENEO LA MAHAKAMANI, MFANYABIASHARA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI BINAFSI IITWAYO AQ CUMPUTER CO.LTD, UPELELEZI UMEBAINI KWAMBA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU AKISHIRIKIANA NA WENZAKE SABA (7) WAMEFANIKIWA KUKUSANYA FEDHA ZAIDI YA TSH 100,000,000/= KUTOKA KWA WANANCHI AMBAO WALISHAWISHIWA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHAKE, PIA UPELELEZI UMEBAINI KUWA AQ POWER CLUB SIO TAASISI ILIYOSAJILIWA KISHERI BALI JINA LA BIASHARA LA MTUHUMIWA.

TAYARI MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU NA WENZAKE SABA WAMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA PINDI UKIKAMILIKA JARADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA DHIDI YAO, AIDHA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA KIKUNDI/ KAMPUNI BINAFSI YA BEGA KWA BEGA MICRO FINANCE COMPANY LTD, KWANI WATU WENGI WAMEKUJA KURIPOTI POLISI JUU YA KUTAPELIWA FEDHA ZAO NA KAMPUNI HIYO, TAYARI JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEWATIA MBARONI WAKURUGENZI NA BAADHI YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI HIYO NA MAJALADA YA KESI HIZO YAPO KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA  KISHERIA.

AIDHA JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUZIFANYIA KAZI TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KUHUSU TAASISI ITAMBULIKAYO KWA JINA LA AMKA MWANAMKE (AMWA), KWAMBA PIA INAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU, UCHUNGUZI UNAFANYWA ILI KUWEZA KUBAINI UKWELI WA TAARIFA HIZO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAWATAHADHARISHA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIEPUSHA NA VIKUNDI VYA AINA HII, PIA ANAWAAASA WANANCHI KUJITAFUTIA KIPATO CHA HALALI KWA KUFANYA KAZI HALALI NA SIO KUWEKEZA FEDHA KIDOGO (KUPANDA) NA KUTARAJIA KUPATA FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI ( MAVUNO). TAMAA YA KUPATA UTAJIRI WA HARAKAHARAKA UMEWAINGIZA WANANCHI WENGI KWENYE HASARA KUBWA ILIYO TOKANA NA KUIBIWA FEDHA ZAO KWANI HAKUNA KIKUNDI/ MTU ANAYEWEZA KUPEWA FEDHA KWA MUDA MFUPI ALAFU BAADA YA MUDA MFUPI ALIPE FEDHA NYINGI ZAIDI. WANANCHI WATAMBUE KUWA HUU NI MTEGO WA WAHALIFU WA KUWAFANYA WANANCHI WASHAWISHIKE KUJIUNGA NA VIKUNDI HIVYO ILI WAWAIBIE.

IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.