ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 23, 2017

SILAHA MOJA YAPATIKANA NA MAJAMBAZI WAWILI KUUAWA WAKATI WAKITAKA KUJARIBU KUTOROKA ASKARI POLISI WILAYANI ILEMELA.

 MAJAMBAZI WAWILI WAUWAWA JIJINI MWANZA.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

WATU wawili wanaosadikika kuwa majambazi Eric Magese (22), na Peter aliyejulikana kwa jina  moja, (25-27), wameuawa huku  silaha moja ikipatikana Jijini hapa wakati wakijaribu kuwatoroka Askari Polisi  walipokuwa wakiwapeleka mahali ambapo wenzao wamejificha ili waweze kufanya uvamizi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Ahmed Msangi amethibitisha kutokea  kwa tukio hilo na kueleza kuwa mnamo january 20,2016  saa 2 Usiku, katika mtaa wa Kiloleli A Kata ya  Nyasaka wilayani Ilemela, Ilipatikana silaha moja aina ya Short Gun yenye namba TZ CAR 103283 ikiwa na risasi tatu ambayo inadaiwa walipora kwenye kampuni ya ulinzi ya Malika Security Servise Limited.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi amesema kuwa Majambazi hao walikuwa wakitafutwa na Polisi baada ya kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo ya kitangiri Disemba 19 mwaka jana,  saa 4 usiku walipovamia duka (Super Market iitwayo Stop na Pax) ambapo walimjeruhi kwa risasi mlinzi lakini hawakufanikiwa kupora kitu chochote.

“Majambazi hao pia walifanya unyang’anyi wa kutumia siraha january 2 mwaka jana saa4 Usiku katika mta wa Nyasaka ambapo walivamia duka la bidhaa mbalimbali mali ya Gasper Johas (40) kisha wakapiga risasi moja hewani na kupora fedha Sh.4 milion" amesema Msangi.

Amefafanua kuwa wakati Askari wakiendelea kuwatafuta majambazi hao zilipatikana taarifa kutoka kwa raia wema aikieleza kuwa wameonekana mjini Mwanza, ndipo Askari waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata  Eric  na alipo hojiwa alikiri kuhusika katika matukio tajwa hapo juu kisha aliwapeleka  nyumbani kwake ambapo kulipatikana silaha hiyo   na kueleza kuwa alikuwa akishirikiana na mwenzake Peter ambaye naye alikamatwa.

Askari waliendelea kuwahoji na ndipo walipoeleza kuwa  walipanga kuvamia maduka mengine Jijini hapa maeneo ya Kirumba wakishirikiana na wenzao wawili ambao majina yao yamehifadhiwa na kwamba watu hao walikubali kuwapeleka askari hadi eneo ambalo walipanga kukutana ili wafanye uvamizi.

Amesema kwamba Majambazi hao walipofika na Askari katika eneo hilo walianza kupiga kelele kama ishara ya kuwatorosha wenzao na kuanza kuwakimbia na ndipo walifyatua risasi kadhaa hewani wakiwaamuru wasimame lakini hawakusimama.

Baada ya kuona hivyo Askari walifyatua risasi za mguuni na kwamba kwa bahati mbaa ziliwalenga maeneo ya juu na kisha kufariki dunia wakati wakipelekwa Hospitalini na miili ya marehemu  imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya  uchunguzi.

Upelelezi na msako bado unaendelea wa kuwakamata  majambazi wengine ambao bado hawajapatikana na Kamanda Msangi ametoa wito kwa wananchi wa Jiji na mkoa wa  Mwanza kuwaelimisha vijana waache tabia ya kujihusisha na uharifu wa kutumia silaha kwani ni kosa la jinai.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.