ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 18, 2017

NUSU YA UTAJIRI WA DUNIA UKO MIKONONI MWA WATU 8.

Nusu ya utajiri wote duniani uko mikononi mwa matajiri wanane tu ambapo mmiliki wa shirika la Microsoft, Bill Gates anaongoza orodha ya matajiri hao. Vilevile ripoti zinasema ufa baina ya watu tajiri na masikini unazidi kupanuka.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Oxfam la Uingereza, ufa baina ya matajiri wakubwa zaidi na watu masikini zaidi umeongezeka kwa viwango vya juu sana. 
Baada ya mmiliki wa Microsoft, matajiri wengine wakubwa duniani ni mwanzilishi wa Kampuni ya Inditex Amancio Ortega, mwekezaji mkongwe Warren Buffett, Carlos Slim wa Mexico, mkuu wa shirika la Amazon, Jeff Bezos, mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg, mmiliki wa Oracle Larry Ellison na meya wa zamani wa New York City Michael Bloomberg.
Ripoti imesema ufa baina ya watu masikini na matajiri ni zaidi ya ilivyodhaniwa hapo kabla na kuongeza kuwa, mtu moja katika kila watu 10 anaishi kwa kipato cha chini ya $2 kwa siku.
Umasikini nchini Marekani.

Mwaka 2016, Oxfam ilitoa ripoti iliyoonesha kuwa matajiri 62 duniani wanamiliki utajiri sawa na unaomilikiwa na nusu ya watu wote duniani.
Nchini Marekani kuliwahi kuibuka harakati ya kukalia "Wall Street" ya kupinga mfumo wa kibepari ambapo wanaharakati hao wanasema kuwa, asilimia moja ya matajiri Wamarekani inawadhulumu asilimia 99 ya wananchi wa nchi hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.